• HABARI MPYA

  Wednesday, February 08, 2017

  MANJI AITWA KUHOJIWA KWA TUHUMA ZA KUUZA DAWA ZA KULEVYA

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  MWENYEKITI wa Yanga, Yussuf Manji na Katibu wa zamani wa Simba, Iddi Azzan ni kati ya watu 65 waliotajwa leo na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kutuhumiwa kujihusisha na biashara ya dawa za kulevya.
  Katika Mkutano wake na waandishi wa Habari mjini Dar es Salaam leo, Makonda aliwataka wote 65 kufika makao makuu ya Jeshi la Polisi Ijumaa kwa mahojiano juu ya tuhuma hizo.
  Hii ni awamu ya pili ya vita ya dawa za kulevya zilizoibuliwa na Makonda na kuungwa mkono na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk John Pombe Magufuli.
  Awali walikamatwa watuhumiwa wa utumiaji, wakiwemo wasanii maarufu ambao nao baada ya mahojiano baadhi yao walipandishwa kizimbani.

  Yussuf Manji naye ametajwa leo katika orodha ya washukiwa wa biashara ya dawa za kulevya

  ORODHA KAMILI YA WALIYOITWA KUHOJIWA IJUMAA  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MANJI AITWA KUHOJIWA KWA TUHUMA ZA KUUZA DAWA ZA KULEVYA Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top