• HABARI MPYA

  Tuesday, February 07, 2017

  MAMBO YAIVA SAUTI ZA BUSARA 2017

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  TAMASHA la Sauti za Busara 2017 liko tayari kutikisa tasnia ya muziki wa Afrika  kwa mfufulizo wa vikao vyenye lengo la kukuza mafunzo ya sanaa. Wataalamu kutoka Dar es Salaam na Dakar watakutanishwa na Movers &  Shakers  na kutoa nafasi kwa viongozi wa  tasnia  ya muziki kukutana na kubadilisha mawazo ya kitaalama.
  Ijumaa kutakua na mada inayohusu fursa za mitandaoni,  changamoto na vitisho vinavuyoigusa tasnia ya muziki. Kutoka kwenye jopo la wageni Jude Clark, mwanzilishi wa  Joose Digital na Eddie Hatitye, Mkurugenzi wa  Music in Africa wataongelea ujuzi wao kwenye maeneo ya hatimiliki, utandawazi, digitali, soko la muziki duniani na maswala ya teknolojia ya mitandao. Kwa kutambua uwezo wa kidigitali ni muhimu kwenye taaluma, wahudhuriaji watashuhudia nguvu ya mitandao ya kijamii ilivyo na nguvu ya kuunganisha mashabiki na wawekezaji, na kuongeza masoko kwa kutumia mitandao ya kijamii.
  Wanamuziki  hujikuta mstari wa mbele kwenye harakati maarufu  kwa kutumia sauti zao kwa niaba ya wasiosikika. Wakati mwingine wasanii hujikuta hatarini baada ya ujumbe wa muziki wao kuwatuhumu wasikilizaji na wenye mamlaka.
  Msanii anawezaje kutumia uhuru wa kuongea  na kufungiwa kitaaluma? Mada ya Jumamosi itaeleza mtazamo huru wa ubunifu Afrika, ripoti imeandikwa na waandishi 25 kutoka Nchi 14 na kuchapishwa  kwa ushirikiano wa Artwatch Afrika kama sehemu ya mtandao wa Arterial, wenye lengo la kulinda uhuru wa kujieleza. Jopo litajumuisha Nelson Mandela wa kundi la Sarabi Kenya, Mamou Daffe – Mkurugenzi,Tamasha la  sur le Niger, Mali na Dr. Omar Abdalla Adam –Mkurugenzi,  Bodi ya Udhibiti Zanzibar.
  Jumapili wasanii wa tamasha wanakaribishwa  kwa maswali na majibu ya kina. Washiriki wanatarajiwa kuwa Pat Thomas and Kyekyeku kutoka Ghana, Roland Tchakounte kutoka Cameroun, Bi Mariam Hamdani kutoka Zanzibar and Sahra Halgan kutoka Somaliland. Hii ni sehemu ya kipekee  kwa wasanii kutoka bara la Afrika na sehemu mbalimbali kukutana na kubadilishana mawazo. Mada  hii itaongozwa na Journey Ramadhan, meneja wa Tamasha.
  Movers & Shakers imeandaliwa kutengeneza nafasi za kipekee kwa wasanii na kuwajengea uwezo ili tasnia ya muziki Afrika Mashariki isonge mbele. Mada zitatolewa kila siku kuanzia saa 8:00 mchana mpaka saa 9:30 jioni . Hotel ya Monsoon. Kuingia ni kwa mwaliko tu. Hovyo wasanii na mameneja  wa ndani  wanahamasishwa kuwasiliana na  waandaaji wa  tamasha la Sauti za Sauti za Busara kama watapenda kushiriki.
  Tamasha la Sauti za Busara 2017 limedhaminiwa na: Ubalozi wa Norway, Shirika la Uswis la Ushirikiana na Maendeleo  (SDC), ZANTEL, Africalia, Ubalozi wa Ujerumani, Zanlink, Memories of Zanzibar, Ethiopian Airlines, Mozeti, Coastal Aviation, Ikala Zanzibar Stone Town Lodge, Music in Africa, Chuchu FM Radio, Tifu TV na Zanzibar Media Corporation.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAMBO YAIVA SAUTI ZA BUSARA 2017 Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top