• HABARI MPYA

  Thursday, February 09, 2017

  LWANDAMINA: YANGA KUTOKUWA NA UWANJA WAKE INANIVURUGIA PROGRAMU ZANGU

  Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
  KOCHA wa Yanga SC, Mzambia George Lwandamina amesema kwamba kitendo cha klabu hiyo kutokuwa na Uwanja wake kinamfanya ashindwe kupangilia vizuri na mapema programu zake.
  Lwandamina alisema hayo jana jioni alipokuwa akizungumzia matayarisho ya timu yake kabla ya kwenda Comoro usiku wa kuamkia Jumamosi kwa ajili ya mchezo wa kwanza Raundi ya Awali ya Ligi Mabingwa Afrika.
  “Silalamikii hilo, kwa sababu ni tatizo la kitaifa. Hata Simba hawana Uwanja, na timu nyingine tu nyingine hapa hazina uwanja, lakini ninasema tu,”alisema.
  Kocha George Lwandamina amesema kwamba Yanga kukosa Uwanja wake inamfanya ashindwe kupangilia vizuri na mapema programu zake

  “Kuna wakati unataka kufanya mazoezi asubuhi, lakini unaambiwa leo uwanja unatumiwa na timu nyingine, inabidi program uihamishie jioni, vitu kama hivyo, lakini tunakabiliana na changamoto hiyo na mambo yanakwenda,”alisema.
  Leo Yanga itafanya mazoezi jioni Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam kabla ya kesho kufanya jioni  tayari kwa safari yao usiku wa kuamkia Jumamosi.  
  Yanga watakuwa wageni wa Ngaya Club Jumapili katika mchezo wa kwanza wa Raundi ya Awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika kabla ya timu hizo kurudiana wiki inayofuata mjini Dar es Salaam.
  Na Lwandamina aliye katika msimu wake wa kwanza Yanga SC tangu arithi mikoba ya Mholanzi, Hans van der Pluijm mapema kesho anatarajiwa kutaka wachezaji watakaokwend Comoro.    
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: LWANDAMINA: YANGA KUTOKUWA NA UWANJA WAKE INANIVURUGIA PROGRAMU ZANGU Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top