• HABARI MPYA

  Monday, February 06, 2017

  LWANDAMINA: UBINGWA, MUNGU NDIYO ANAJUA

  Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
  KOCHA wa Yanga, Mzambia George Lwandamina amesema kwamba Mungu pekee ndiye anajua nani atakuwa bingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara msimu huu.
  Mzambia huyo aliyeanza kazi Yanga SC Novemba mwaka jana, alisema hayo jana katika mazungumzo na Bin Zubeiry Sports - Online baada ya kuombwa tathmini yake juu ya mbio za ugingwa wa Ligi Kuu kwa sasa.
  Yanga inaongoza Ligi Kuu kwa pointi zake 49 baada ya kucheza mechi 21, ikifuatiwa na watani wa jadi, Simba SC wenye pointi 48 za mechi 21 pia.
  Na baada ya timu zote kushinda vizuri mechi zao za wikiendi, Yanga ikiifunga Stand United 4-0 Dar es Salaam na Simba ikiifunga Maji Maji 3-0 Songea – sasa zitakutana zenyewe Februari 25.
  Na kuelekea mchezo huo, Lwandamina amesema; “Siwezi kuzungumzia mchezo huo, bado ni mapema sana,”.
  Lakini akakataa pia kutoa tathmini yake juu ya mbio za ubingwa baada ya timu zote kushinda wikiendi hii akisema; “Siwezi kusema chochote juu ya hilo, ni Mungu pekee ndiye ajuaye,”alisema.   
  Baada ya kuitandika Stand United 4-0 mabao ya Donald Ngoma, Simon Msuva, Obrey Chirwa na Nahodha Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Yanga itasafiri Ijumaa kwenda Comoro kwa ajili ya mchezo wa kwanza wa Raundi ya Awali Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya wenyeji, Ngaya Club.
  Watacheza Jumapili Comoro kabla ya kurudiana juma linalofuata Dar es Salaam na baada ya hapo watakwenda mafichoni kwa ajili ya mchezo dhidi ya Simba, Februari 25. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: LWANDAMINA: UBINGWA, MUNGU NDIYO ANAJUA Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top