• HABARI MPYA

  Thursday, February 02, 2017

  LAMPARD ASTAAFU RASMI SOKA BAADA YA MIAKA ZAIDI YA 20

  KIUNGO Frank Lampard ametangaza kustaafu soka ya ushindnai baada ya zaidi ya miongo miwili ya kuwa kazini.
  Gwiji huyo wa Chelsea, ambaye alishinda heshima zote kubwa wakati wake akiwa kazini Stamford Bridge, ameamua kustaafu baada ya kuondoka New York City ya Ligi Kuu ya Marekani mwishoni mwa msimu.
  Lampard, mwenye umri wa miaka 38 sasa, ametangaza kustaafu kwake kupitia ukurasa wake wak Instagram ambako ameposti ujumbe wa kuwashukuru wote waliochangua mafanikio yake ikiwemo kuichezea mechi 106 timu yake ya taifa ya England.
  Kiungo wa zamani wa Chelsea na England ametangaza kustaafu soka 

  HISTORIA YA LAMPARD 

  1995-2001: West Ham - mechi 187/mabao 39
  1995-96: Swansea (mkopo) - mechi 11/bao 1
  2001-2014: Chelsea - mechi 649/mabao 211
  2014-15: Man City - mechi 38/mabao 8
  2015-16: New York City - mechi 19/mabao 12
  1999-2014: England - mechi 106/mabao 29 
  JUMLA: mechi 1010/mabao 300

    

  MATAJI ALIYOTWAA LAMPARD

  Chelsea
  Ligi Kuu x3: 2004-05, 2005-06, 2009-10
  Kombe la FA x4: 2006-07, 2008-09, 2009-10, 2012
  Kombe la Ligi x2: 2004-05, 2006-07 
  Ngao ya Jamii
  x2: 2005, 2009
  Ligi ya Mabingwa: 2011-12
  Europa League: 2012-13  
  West Ham
  Intertoto Cup: 1999  

  Lampard ameishukuru familia yake, akiwemo mkewe Christine ambaye ameandika ujumbe wa kujivunia mumewe kwenye ukurasa wake wa Instagram pamoja na picha ya 'bwana mkubwa huyo'.
  Lampard amezishukuru pia klabu alizochezea enzi zake kuanzia West Ham katikati ya miaka tisini. Amesema Chelsea, ambako ameshinda mataji matatu ya Ligi Kuu ya England, mannde ya FA na Ligi ya Mabingwa Ulaya zaidi ya miaka 13 daima itabakia kuwa na nafasi kubwa moyoni mwake na pia akazishukuru Manchester City na New York City. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: LAMPARD ASTAAFU RASMI SOKA BAADA YA MIAKA ZAIDI YA 20 Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top