• HABARI MPYA

  Tuesday, February 07, 2017

  KOSCIELNY APONDA UPANGAJI WA TIMU WA WENGER ARSENAL

  BEKI wa Arsenal, Laurent Koscielny amejitolea kukooa upagaji wa timu wa kocha Arsene Wenger kufuatia kipigo cha The Gunners hivi karibuni Uwanja wa Stamford Bridge.
  Kikosi cha Wenger kilisambaratishwa na vinaraa wa Ligi Kuu, Chelsea katika kipigo ambacho kimepunguza mno matumaini ya ubingwa kwao.
  Na mwanasoka huyo wa kimataifa wa Ufaransa, Koscielny amezungumzia upangwaji wa timu siku hiyo London Kaskazini uliowaruhusu The Blues kuongoza Ligi Kuu ya England kwa pointi 12 zaidi.

  Laurent Koscielny (kulia) ameponda upangaji wa timu wa Wenger katika mchezo dhidi ya Chelsea PICHA ZAIDI GONA HAPA  

  "Nafikiri tuliwachezesha wachezaji tofauti na tuliopaswa kuwachezesha na ninafikiri tulipaswa kucheza kitimu zaidi na kulikuwa kuna nafasi ya kufanya hivyo. Walitupiga kwa mashambulizi ya kushitukiza,"alisema Koscielny.
  Wenger alipanga kikosi cha aina yake katika mchezo huo, akiwaanzisha Theo Walcott na Mesut Ozil badala ya Danny Welbeck na nyota wa timu, Alexis Sanchez na wakafungwa na Chelsea 3-1 Uwanja wa Stamford Bridge.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KOSCIELNY APONDA UPANGAJI WA TIMU WA WENGER ARSENAL Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top