• HABARI MPYA

  Thursday, February 09, 2017

  KAGERA SUGAR KUCHEZA NA LIPULI KUMCHANGIA MAREHEMU BURHAN

  Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
  TIMU ya Kagera Sugar ya Bukoba keshokutwa itacheza mchezo maalum wa kirafiki na wenyeji Lipuli Uwanja wa Samora, Iringa kumchangia aliyekuwa kipa wake, David Burhan aliyefariki dunia Januari 30, mwaka huu mjini Mwanza.  
  Akizungumza na Bin Zubeiry Sports – Online leo, kocha wa Kagera Sugar, Mecky Mexime alisema kwamba wataondoka Bukoba kesho mapema kwenda Iringa kwa ajili ya mchezo huo.
  Mexime alisema kwamba wameamua kucheza mechi huyo maalum ili kuichangia fedha familia ya marehemu.
  “Kama unavyojua, familia yake ilikuwa inamtegemea na sasa hayupo tena, kwa hivyo tukafikiria kwa pamoja na kupata wazo la kucheza hiyo mechi ili kuwapatia fedha,”alisema. 
  David Burhan alifariki dunia Januari 30, mwaka huu mjini Mwanza

  Baada ya mchezo huo, Kagera Sugar itakwenda Mbeya ambako Februari 15 itacheza mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya wenyeji, Prisons. 
  Burhan, kipa bora wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara msimu wa 2013/2014, David alifariki dunia asubuhi ya Januari 30, mwaka huu katika hospitali ya Bugando, Mwanza, siku moja tu baada ya kufikishwa hospitalini hapo kwa matibabu kutoka Bukoba.
  Burham alijiunga na Kagera Sugar msimu huu akitokea Maji Maji ya Songea, ambayo nayo ilimtoa Mbeya City. Huyo ndiye aliyekuwa kipa wa kwanza Mbeya City wakati inapanda Ligi Kuu misimu mitatu iliyopita chini ya kocha Juma Mwambusi na akawa kipa bora wa msimu wa 2013/2014.    
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KAGERA SUGAR KUCHEZA NA LIPULI KUMCHANGIA MAREHEMU BURHAN Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top