• HABARI MPYA

  Saturday, February 04, 2017

  GABON WENYEJI WAPYA U-17 AFRIKA, GHANA YAWANIA NAFASI YA TATU AFCON KUBWA LEO

  SHIRIKISHO la Soka Afrika (CAF) imeiteua Gabon kuwa mwenyeji wa Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa vijana chini ya umri wa miaka 17, kuchukua nafasi ya Madagascar iliyopokonywa uenyeji mwezi uliopita.
  Uamuzi huo ulifanywa jana katika kikao cha Kamati ya Utendai ya CAF kilichofanyika katika hoteli ya Raddison Blu kueleka fainali ya AFCON ya wakubwa 2017 Afcon kati ya Cameroon na Misri.
  Mapema mwezi huu, Kamati ya Utendaji ya CAF iliipokonya ghafla uenyeji Madagascar baada ya kubaini hawakutimiza vigezo.
  Michuano hiyo itatoa timu nne ambazo zitaiwakilisha Afrika kwenye Kombe la Dunia la FIFA chini ya umri wa miaka 17 itakaofanyika nchini India baadaye mwaka huu. Niger walikuwa wenyeji wa Afcon iliyopita ya U-17 mwaka 2015 na Mali wakatwaa ubingwa.
  Wakati huo huo: Burkina Faso inaamenyana na Ghana leo Uwanja wa Port Gentil kuanzia Saa 4:00 usiku katika mchezo wa kuwania nafasi ya tatu ya AFCON ya wakubwa.
  Ikumbukwe AFCON ya mwaka huu nchini Gabon itafungwa kesho kwa mchezo wa fainali kati ya Misri na Cameroon kuanzia Saa 4:00 usiku pia.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: GABON WENYEJI WAPYA U-17 AFRIKA, GHANA YAWANIA NAFASI YA TATU AFCON KUBWA LEO Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top