• HABARI MPYA

  Saturday, February 18, 2017

  ETI KISARAFU NDIYO KIMEWANYIMA MABAO YANGA LEO DHIDI YA NGAYA

  Wachezaji wa Ngaya de Mde ya Comoro wakiwa wameshika mshambuliaji wa Yanga, Obrey Chirwa (katikati) baada ya kwenda kutoa sarafu kwenye lango lao wakati wa mchezo wa marudiano baina ya timu hizo Raundi ya Awali Ligi ya Mabingwa Afrika jioni ya leo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Timu hizo zimetoka sare ya 1-1 na Yanga imesonga mbele kwa ushindi wa jumla wa 6-2 baada ya wiki iliyopita kushinda 5-1 ugenini mjini Moroni, Comoro.  
  Chirwa alipambana asipokonywe sarafu hiyo 
  Wachezaji wa Ngaya walijitahidi kumpokonya sarafu hiyo bila mafanikio
  Lakini hawakukata tamaa, walihakikisha wanamdhibiti vizuri ili aiachie
  Alipoona anakaribia kuzidiwa nguvu, Chirwa akaitupa nje sarafu hiyo 
  Baada ya kuitupa nje akaamini sasa ugumu wa kupata mabao utaisha
  Hapa anawaambia; "Sarafu yenu inaayotuzuia tusiwafunge mabao ilee" pichani chini 

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: ETI KISARAFU NDIYO KIMEWANYIMA MABAO YANGA LEO DHIDI YA NGAYA Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top