• HABARI MPYA

    Wednesday, February 01, 2017

    EL HADARY AWANIA BONGE LA REKODI LEO AFCON

    KIPA wa Misri, Essam El Hadary alishinda taji lake la kwanza la Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka 1998 wakati mchezaji mwenzake wa sasa, Ramadhan Sobhi ana umri wa mwaka mmoja.
    Kutokana na kudumu kwake kwenye soka ya ushindani kwa muda mrefu, amejikuta anacheza na vijana ambao wanaweza kuwa watoto wake wa kuwazaa mweneywe.
    “Ramadan Sobhi ana umri karibu sawa na mwanangu wa kike, lakini nawachukulia kama wote kama wachezaji wenzangu kama wadogo zangu na ninamchukulia kama mchezaji mwenzangu,” alisema El Hadary.
    Essam El Hadary anawania kushinda taji la tano la Kombe la Mataifa ya Afrika  

    El Hadary ni mchezaji pekee kwenye kikosi cha sasa cha Misri aliyekuwa kwenye kikosi kilichoifunga Afrika Kusini mwaka 1998 katika fainali ya AFCON nchini Burkina Faso na wakati anaingia kuwavaa Etalons usiku wa leo katika Nusu Fainali, atawania kuingia fainali akatwae taji la tano la AFCON.
    “Ni vizazi tofauti pamoja na hayo, kila kizazi kina haina na desturi zake. Nimeshinda mataji manne ya Afcon na vizazi vilivyopita, kwa sababun tumekuwa pamoja na kutwaa mataji manne.”
    “Pamoja na hayo, nikiwa na kizazi hiki kipya, hawajatwaa taji la Afcon. Wakati wote nawaambia hadithi na namna tulivyoweza kufanya hivyo,".
    “Tumejituma hadi kufika hatua hii na kwa pamoja kama timu tutaweza kushinea taji na safari inaanzia dhidi ya Burkina Faso,"alisema.
    El Hadary hajafungwa hata bao moja katika Afcon ya 2017 na anatarajiwa kuendeleza rekodi hiyo usiku wa leo katika Nusu Fainali dhidi ya Burkina Faso kuanzia Saa 4:00 usiku uwanja wa d'Angondje mjini Libreville, Gabon. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: EL HADARY AWANIA BONGE LA REKODI LEO AFCON Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top