• HABARI MPYA

  Thursday, February 02, 2017

  EL HADARY ACHEZA PENALTI MBILI NA KUIPELEKA MISRI FAINALI

  KIPA mwenye umri wa miaka 44, Essam El-Hadary usiku wa jana aliibuka shujaa wakati Misri ikitinga fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika kwa kuitoa Burkina Faso kwa penalti 4-3 kufuatia sare yaa 1-1 ndani ya dakika 120 Uwanja wa de I'Amitie mjini Libreville, Gabon.
  Misri walitangulia kwa bao la Mohamed Salah dakika ya 65 kaabla ya Aristide Bance kuisawazishia Burkina Faso dakika saba baadaye.
  Kipa mkongwe,  El-Hadary akathibitisha ushujaa wake kwa kwenda kjuokoa mikwaju miwili ya penalti ya kipa mwenzake Kouakou Herve Koffi na mshambuliaji Bertrand Isidore Traore.  

  Kipa Essam El-Hadary akiwa amezingirwa na wachezaji wenzake kupongezwa baada ya kuiwezesha Misri kwenda fainali ya AFCON
   
  PICHA ZAIDI GONGA HAPA  

  Wachezaji wa Burkina Faso waliomfunga Hadary ni Alain Traore, Banou Diawara na Steeve Yago, wakati waliofunga penalti za Misri ni Ramadan Sobhi, Ahmed Hegazi, Mohamed Salah na Amr Warda baada ya Abdalla El Said kukosa ya kwanza.
  Sasa mabingwa mara saba Afrika, Mafarao wa Misri watakutana na mshindi kati ya Ghana na Cameroon zinazomenyana usiku wa leo kwenye Nusu Fainali ya pili katika fainali Jumapili.
  Kikosi cha Misri kilikuwa: El-Hadary, El Mohamady/Gaber dk106, Hegazy, Gabr, Fathy, Hamed, M. Salah, I. Salah, Said, Trezeguet/Sobhi dk85 na Kahraba/Warda dk76.
  Burkina Faso: Koffi, Yago, Dayo, B. Kone, Y. Coulibaly, Kabore, I. Toure, R. Traore/Diawara dk80, B. Traore, Bance/A.Traore dk102 na Nakoulma.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: EL HADARY ACHEZA PENALTI MBILI NA KUIPELEKA MISRI FAINALI Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top