• HABARI MPYA

  Tuesday, February 07, 2017

  DIOUF AWAKANDIA JOE MATIP NA WENZAKE KUGOMA KUICHEZEA CAMEROON AFCON

  MWANASOKA bora wa zamani Afrika, El-Hadj Diouf amewaambia wachezaji wanane waliogoma kuichezea Cameroon kwenye Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka huu watajutia uamuzi wao.
  Nyota huyo wa zamani wa Senegal ameshangaa mno wachezaji wengi tegemeo wa Simba Wasiofungika walikataa kuichezea yao, na sasa watajutia baada ya wenzao kwenda kuipigani timu na kutwaa Kombe nchini Gabon.
  Joe Matip wa Liverpool, Eric Choupo-Moting wa Schalke na Allan Nyom wa West-Bromwich-Albion, ndiyo wachezaji wakubwa zaidi waliojitoa kikosini na Diouf amewashauri, akirejea wimbo wa gwiji wa Reggae, hayati Bob Marley kuwapa ujumbe.
  El-Hadj Diouf amewaambia wachezaji waliogoma kuichezea Cameroon kwenye Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka huu watajutia uamuzi wao

  "Sielewi kwa nini watu wanazikana nchi zao. Na kama gwiji Bob Marley wakati wote nasema; "Ikiwa hujui ulipotoka, basi hujui pia unapokwenda,"alisema akirejea mistari ya wimbo wa marehemu Bob.
  Wengine ni Andre Onana wa Ajax Amsterdam, Guy Roland Ndy Assembe wa Nancy, Maxime Poundje wa Girondins-Bordeaux, Andre-Frank Zambo Anguissa wa Olympique-Marseille na Ibrahim Amadou wa Lille.
  Simba Wasiofungika waliwafunga Black Stars ya Ghana 2-0 Alhamisi iliyopita kwenye Nusu Fainali kabla ya kwenda kuwafunga 2-0 na Misri katika fainali Jumapili mjini Libreville kutwaa Kombe.
  Diouf amesema hakuna mzamiaji katika soka ya Ulaya amekuwa wa kudumu katika klabu saba na amewataka wachezaji hao kuamini Afrika ndiyo kipaumbele chao na asili yao. 
  "Wazi watajuta kutocheza Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika. Baaada ya kustaafu, utakwenda kufanya nini? Kubaki unaishi Ulaya? Kufanya nini?”
  "Wakati wote ni ngumu kuwa Mwafrika, kwa sababu unaweza kuwa kocha bora Mwafrika, lakini hawawezi kukupa Paris St Germain (PSG), Barcelona, Liverpool au Manchester United."
  "Ndiyo maana nawaambia hao vijana: usiikane nchi yako, kwa sababu msingi wa hii dunia upo Afrika,"alisema.
  Kikosi cha Cameroon kilichotwaa taji la AFCON mwaka huu kiliundwa na makipa; Jules Goda (Ajaccio, Ufaransa), Fabrice Ondoa (Sevilla, Hispania) na Georges Bokwe (Coton Sport, Cameroon).
  Mabeki; Fai Collins (Standard Liege, Ubelgiji), Ernest Mabouka (MSK Zilina, Slovakia), Nicolas Nkoulou (Lyon, Ufaransa), Michael Ngadeu (Slavia Prague, Jamhuri ya Czech), Adolph Teikeu (Sochaux, Ufaransa), Ambroise Oyongo (Impact Monreal, Marekani), Mohammed Djetei (Terragone, Hispania) na Jonathan Ngwen (FC Progresso).
  Viungo ni Sébastien Siani (Oostende, Ubelgiji), Franck Boya (Apejes, Cameroon), Georges Mandjeck (Metz, Ufaransa), Arnaud Djoum (Hearts, Scotland) na washambuliaji Vincent Aboubakar (Besiktas, Uturuki), Jacques Zoua (Kaiserslautern, Ujerumani), Benjamin Moukandjo (Lorient, Ufaransa), Clinton Njie (Olympique Marseille, Ufaransa), Edgar Salli (Nuremberg, Ujerumani), Christian Bassogog (Aalborg, Denmark), Toko Ekambi (Angers, Ufaransa) na Ndip Tambe (Spartak Trnava, Slovakia).
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: DIOUF AWAKANDIA JOE MATIP NA WENZAKE KUGOMA KUICHEZEA CAMEROON AFCON Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top