• HABARI MPYA

  Monday, February 06, 2017

  CAMEROON WATWAA NDOO YA AFRIKA, WAIPIGA 2-1 MISRI

  CAMEROON ndiyo mabingwa wa Afrika, baada ya kuichapa Misri kwa mabao 2-1 usiku wa jana mjini  Libreville, Gabon katika fainali kali ya Kombe la Mataifa barani (AFCON).
  Shukrani kwake Vincent Aboubakar aliyetokea benchi kwenda kuifungia bao la ushindi Cameroon zikiwa zimebaki dakika mbili mchezo kumalizika.
  Kiungo wa Arsenal, Mohamed Elneny aliwafungia bao la kuongoza Misri dakika ya 22 na kuwapa matumaini ya kubeba taji lao la kwanza la AFCON tangu mwaka 2010.
  Lakini Nicolas Nkoulou aliyetokea benchi pia kipindi cha kwanza, akawafungia Simba Wasiofungika bao la kusawazisha dakika ya 59, kabla ya Aboubakar kufunga la ushindi dakika ya 88.

  Na hilo linakuwa taji la tano la Kombe la Mataifa ya Afrika kwa Simba Sasiofungika na la kwanza tangu mwaka 2002 na pia hii ni mara ya kwanza wanaifunga Misri katika fainali.
  "Nina furaha tumeshinda Kombe la Mataifa ya Afrika na ninawafurahia wachezaji -- hili si kundi la wachezaji wa mpira, hili ni kundi la marafiki," alisema kocha Mbelgiji wa Cameroon, Hugo Broos.
  Kikosi cha Cameroon kilikuwa: Fabrice Ondoua, Michael Ngadeu-Ngadjui, Collins Fai, Adolphe Teikeu/Nicolas N’Koulou dk32, Ambroise Oyongo, Sébastien Siani, Arnaud Sutchuin Djoum, Benjamin Moukandjo, Robert Ndip Tambe/Vincent Aboubakar dk46, Christian Bassogog na Jacques Zoua/Georges Mandjeck dk90+4.
  Misri: Essam El Hadary, Ahmed Fathi, Ahmed Hegazy, Ali Gabr, Ahmed Elmohamady, Mohamed Elneny, Tarek Hamed, Amr Warda, Abdallah Said, Mahmoud Hassan/Ramadan Sobhi dk66 na Mohamed Salah.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: CAMEROON WATWAA NDOO YA AFRIKA, WAIPIGA 2-1 MISRI Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top