• HABARI MPYA

  Thursday, February 16, 2017

  BARNABAS AJIANDAA KUSTAAFU, AENDA KUSOMEA UKOCHA

  Na Mwandishi Wetu, MOROGORO
  WINGA mkongwe aliyeitumikia Mtibwa Sugar na timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars kwa muda mrefu, Vincent Barnabas Saramba ameanza maandalizi ya kutungika daluga zake kwa kuamua kusomea ukocha.
  Akizungumza na Bin Zubeiry Sports – Online leo, Barnabas aliyewahi kuchezea vigogo wa Tanzania pia, Yanga SC amesema kwamba anatarajia kuanza kusomea ukocha baada ya kupewa baraka zote na uongozi wa Mtibwa Sugar.
  “Ninatarajia kwenda kusomea kozi hiyo ya ukocha mjini Morogoro, mafunzo hayo ya ukocha wa awali yatanichukua muda wa wiki mbili,”alisema Barnabas aliyeahi pia kuchezea Kagera Sugar.
  Vincent Barnabas (kushoto) akiwa na wachezaji wenzake wa Taifa Stars mwaka 2013 Juma Kaseja (kulia) na Shomary Kapombe (katikati) 

  Kwa upande wake, Mratibu wa Mtibwa Sugar, Jamal Bayser amethibitisha kumpa baraka zote winga huyo kwenda kusomea ukocha.
  “Huu ni mwendelezo wa utamaduni wetu wa kuwsomesha  ukocha wachezaji wetu wanaostaafu, kama itakumbukwa Mtibwa Sugar pia iliwasomesha akina Salum Mayanga, Zubery Katwila, Edwin Hagai, Salhina Mjengwa na Mecky Mexime,”.
  Wakati huo huo, katika kujiandaa na mchezo ujao wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Mtibwa Sugar imepokea habari njema ambayo ni kurejea kwa Nahodha wake Msaidizi, Salim Mbonde aliyekuwa anasumbuliwa na Malaria na kuwa nje ya Uwanja kwa takriban wiki tatu.
  Mbonde, kisiki imara cha safu ya ulinzi ya Mtibwa Sugar, hakuwepo wakati timu hiyo inafungwa 2-1 na Kagera Sugar Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba, 5-0 na Mbao FC Uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza na kutoa sare ya 2-2 na African Lyon Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.
  Daktari wa timu, Mussa Juma ameiambia Bin Zubeiry Sports – Online kwamba Mbonde yuko fiti kwa ajili ya mchezo ujao dhidi ya JKT Ruvu Uwanja wa Manungu, Turiuani mkoani Morogorio.
  Daktari huyo mzoefu alisema kuwa mchezaji pekee anayeendekea kubaki ‘wadi ya wagonjwa’ manungu ni Said Mkopi ambaye yuko nje ya uwanja kwa takribani miezi miwili sasa akiuguza goti.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: BARNABAS AJIANDAA KUSTAAFU, AENDA KUSOMEA UKOCHA Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top