• HABARI MPYA

  Sunday, February 12, 2017

  AZAM FC KUCHEZA NA RED ARROWS JUMATANO CHAMAZI

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  TIMU ya Azam FC inatarajiwa kushuka tena dimbani Jumatano ijayo kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Red Arrows ya Zambia Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
  Arrows imekuja nchini kuweka kambi maalumu ya maandalizi ya msimu mpya wa Ligi Kuu ya Zambia, utakaoanza saa 1.00 usiku ndani ya Uwanja wa Azam Complex.
  Azam FC itautumia mchezo huo kama sehemu ya maadalizi ya michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika, ambapo inatarajia kufungua pazia mwezi ujao kwa kukipiga na mshindi wa jumla wa mechi ya raundi ya awali kati ya Orapa United ya Botswana na Mbabane Swallows ya Swaziland.
  Arrows iliyowahi kufundishwa na Kocha wa Yanga, George Lwandamina kabla ya kutimkia Zesco United, ipo nchini chini ya wenyeji wao Azam FC, ambapo wamekuwa wakitumia miundombinu ya timu hiyo ndani ya makao makuu yake ya Azam Complex, kwa kufanyia mazoezi tokea iwasili nchini mwanzoni mwa wiki hii.
  Wakati huo huo: Azam FC jana ilitoka sare ya bila kufungana na wenyeji wao, Ruvu Shooting katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) uliofanyika Uwanja wa Mabatini, Mlandizi, Pwani jioni ya leo.
  Sare hiyo imeifanya Azam FC kufikisha jumla ya pointi 38 katika nafasi ya tatu kwenye msimamo, ikizidiwa pointi 13 na vinara Simba waliofikisha pointi 51 baada ya kuichapa Tanzania Prisons mabao 3-0.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AZAM FC KUCHEZA NA RED ARROWS JUMATANO CHAMAZI Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top