• HABARI MPYA

  Wednesday, February 08, 2017

  ALLAN NYOM ASEMA HAJUTII KUIKANA CAMEROON AFCON

  BEKI wa West Brom, Allan Nyom amesema hajutii kukataa kwenda kuichezea Cameroon na kubaki na klabu yake, West Brom.
  Cameroon iliifunga Misri na kubeba taji la Kombe la Mataifa ya Afrika Jumapili na Nyom alikuwa miongoni mwa wachezaji kadhaa walikataa kwenda kuichezea nchi yao kwenye michuano hiyo nchini Gabon.
  Wengine ni pamoja na Joel Matip aliyeamua kubaki na Liverpool nchini England, huku kocha wa Cameroon, Hugo Broos akisema: "Labda wanazugumza wenyewe kwa sasa, 'S***!Kwa nini sikwedna nao?'
  Nyom amesema hajutiii uamuzi wake. wa kutokwenda kuichezea Caeoon

  "Ni kweli, mwanzoni sikutaka kwenda, lakini ya baada ya muda nikabadili mawazongo yangu,".
  "Hata kama kabla ya mashindano wangeniambia Cameroon inakwenda kutwaa Kombe na haumo kikosini, nisingejali kwa sababu nina furaha nachezea klabu, ambayo ni muhimu zaidi kwangu,"alisema
  Alipoulizwa ujumbe wake kwa kocha Broos, Nyom alisema: 'Hongera zake.'
  West Brom inashika nafsi ta sita katika msimamo wa Ligi Kuu ya England na Jumamosi watakuwa wageni wa West Ham Uwanja wa London.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: ALLAN NYOM ASEMA HAJUTII KUIKANA CAMEROON AFCON Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top