• HABARI MPYA

    Monday, February 13, 2017

    AL AHLY YAWAPIGA WAGHANA 3-1 KWAO LIGI YA MABINGWA

    VIGOGO wa Libya, Al Ahly jana wameanza vyema michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kuifunga mabao 3-1 ugenini Wa All Stars ya Ghana.
    Hiyo ilikuwa katika mchezo wa kwanza wa Raundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika jana nchini Ghana.
    Lakini ushindi mkubwa zaidi kwa mechi jana waliupata vigogo wa Tanzania, Yanga SC walioichapa Ngaya Club mabao 5-1 nchini Comoro.
    Mechi nyingine za jana, Coton Sport ya Cameroon iliifunga Atlabara ya Sudan Kusini 2-0 nyumbani, sawa an AC Leopards, Barrack Young Controllers na Gambia Ports Authority, ambao wote walishinda 1-0 nyumbani dhidi ya USM, Stade Malien na Sewe Sports.
    Timu hizo zote tatu zilizofungwa Cameroon, Mali na Ivory Coast zitajaribu kupindua matokeo katika michezo ya marudiano wikiendi nyumbani. 
    Mchezo mwingine, Ela Nguema ya Equatorial Guinea iliwabana vigogo wa Sudan, El- Merreikh kwa sare ya bila kufungana mjini Malabo.
    Mechi za marudiano zinatarajiwa kuchezwa Februari 17 na 19 mwaka huu.

    MATOKEO YOTE MECHI ZA KWANZA RAUNDI YA AWALI LIGI YA MABINGWA AFRIKA KWA UJUMLA: 
    Jumapili Februari 12, 2017
    Ngaya Club 1-5 Yanga SC
    Wa All Stars 1-3 Al Ahly Tripoli
    Coton Sport 2-0 Atlabara
    AC Leopards 1-0 USM de Loum
    Barrack Young Controllers 1-0 Stade Malien
    Gambia Ports 1-0 Sewe Sports
    Ela Nguema 0-0 Al-Merrikh
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: AL AHLY YAWAPIGA WAGHANA 3-1 KWAO LIGI YA MABINGWA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top