• HABARI MPYA

  Saturday, January 07, 2017

  ZIMAMOTO YAIPELEKA AZAM NUSU FAINALI MAPINDUZI

  Na Mwandishi Wetu, ZANZIBAR
  AZAM FC imefanikiwa kufuzu Nusu Fainali ya Kombe la Mapinduzi, baada ya Zimamoto kuifunga Jamhuri 2-0 jioni ya leo katika mchezo wa Kundi B Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
  Matokeo haya yanafanya moja kwa moja Azam iungane na Yanga kwenda Nusu Fainali kutoka Kundi B, baada ya Zimamoto kumaliza na pointi tatu na Jamhuri pointi moja.
  Katika mchezo huo, mabao ya Zimamoto yamefungwa na Hassan Ali dakika ya saba kwa kichwa, akimalizia krosi ya Rashid Ali na la pili dakika ya 59 mfungaji Ibrahim Ahmada baada ya kutokea piga nikupige langoni mwa Jamhuri. 
  Mchezo wa baadate usiku kati ya Azam na Yanga utakuwa tu wa kutafuta mshindi wa kwanza na wa pili wa kundi hilo, baada ya timu zote kufuzu mapema.
  Hatua ya makundi ya michuano ya Kombe la Mapinduzi inahitimishwa kesho kwa michezo miwili ya Kundi A, Simba na Jang'ombe Boys kuanzia Saa 10:00 jioni na URA na Taifa Jang'ombe utakaofuatia Saa 2:30 usiku.
  Hadi sasa hakuna timu yenye uhakika wa Nusu Fainali katika Kundi hilo, ikiwa URA inaweza kufikisha pointi saba za Simba na Jang’ombe Boys na Taifa Jang’ombe wote wanaweza kumaliza na pointi tisa kila mmoja.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: ZIMAMOTO YAIPELEKA AZAM NUSU FAINALI MAPINDUZI Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top