• HABARI MPYA

  Tuesday, January 03, 2017

  ZAHOR PAZI APANIA MAKUBWA MBEYA CITY

  Na Mwandishi Wetu. DAR ES SALAAM
  MSHAMBULIAJI mpya wa Mbeya City, Zahor Pazi amesema kwamba anataka kuitumia timu hiyo kujirudisha juu kisoka baada ya kupotea kwa misimu miwili iliyopita.
  Akizungumza na Bin Zubeiry Sports - Online jana, Pazi mtoto wa kipa wa zamani wa kimataifa wa Tanzania, Iddi Pazi 'Father' alisema kwamba ana hasira za kutocheza soka kwa miaka miwili kufuatia Hati yake ya Uhamisho wa Kimataifa (ITC) kukwama kwa muda mrefu Jamhuri ya Kidemiokrasia ya Kongo (DRC).
  Zahor Pazi anataka kuitumia Mbeya City kujirudisha juu kisoka

  “Hasira zangu za kutocheza soka kwa miaka miwili nataka kuzitumia kwa kujibidiisha hapa Mbeya City ili nirudi juu,”alisema.
  Na Zahor alisema hayo baada ya kufunga bao moja katika mechi yake ya kwanza Jumamosi, Mbeya City wakiilaza 3-1 Mbao FC Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.   
  Mabao mengine ya MCC inayofundishwa na Mmalawi, Kinnah Phiri yamefungwa na Rapahel Alpha na Tito Okelo na kuifanya ifikishe pointi 24 baada ya kucheza mechi 18 na kupanda hadi nafasi ya sita.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: ZAHOR PAZI APANIA MAKUBWA MBEYA CITY Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top