• HABARI MPYA

  Sunday, January 15, 2017

  YANGA YATUA SALAMA SONGEA, KAZI NI JUMANNE MAJI MAJI

  Na Mwandishi Wetu, SONGEA
  KIKOSI cha Yanga SC kimefika salama Songea leo tayari kwa mchezo wake wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara Jumanne Uwanja wa Maji Maji mjini Songea.
  Wachezaji watano tu wanakosekana kwenye kikosi kilichowasili leo jioni mjini Songea, beki Vincent Bossou ambaye yuko Gabon na timu yake ya taifa, Togo, mshambuliaji Mzimbabwe Donald Ngoma na viungo Wazambia Justin Zulu, Obrey Chirwa ambao wote ni majeruhi na Emmanuel Martin aliyekwenda kwenye msiba wa mdogo wake Tanga.
  Kocha Mzambia, George Lwandamina amebeba kikosi kipana kikiongozwa na makipa; Deo Munishi ‘Dida’, Ally Mustafa 'Barthez' na Benno Kakolanya, mabeki Hassan Kessy, Juma Abdul, Mwinyi Mngwali, Oscar Joshua, Andrew Vincent ‘Dante’, Pato Ngonyani, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ na Kevin Yondan.
  Viungo ni Said Juma ‘Makapu’, Thabani Kamusoko, Haruna Niyonzima, Juma Mahadhi, Deus Kaseke, Simon Msuva, Yussuf Mhilu, Geoffrey Mwashiuya na washambuliaji Amissi Tambwe, Malimi Busungu na Matheo Anthony. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA YATUA SALAMA SONGEA, KAZI NI JUMANNE MAJI MAJI Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top