• HABARI MPYA

  Thursday, January 12, 2017

  YANGA YASEMA HAINA MPANGO WA KUACHANA NA LWANDAMINA

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  UONGOZI wa Yanga umesema kwamba hauna mpango wa kumfukuza kocha wake, Mzambia George Lwandamina baada ya timu kutolewa kwenye Nusu Fainali ya Kombe la Mapinduzi.  
  Akizungumza na Waandishi wa Habari jana, Katibu wa Yanga, Baraka Deusdedit alisema kwamba uongozi unaridhishwa na kazi ya Lwandamina hadi sasa licha ya timu kutolewa katika Nusu Fainali ya Kombe la Mapinduzi.
  “Tunashangazwa na taarifa za kizushi kwamba Lwandamina anafukuzwa, afukuzwe kwa sababu gani. Hakuna kitu kama hicho. Lwandamina bado yupo, na ataendelea kuwapo,”alisema Baraka.
  Yanga Imesema haIna mpango wa kumfukuza kocha wake, Mzambia George Lwandamina  

  Uvumi wa kwamba Lwandamina anafukuzwa Yanga ulianza kuzagaa juzi baada ya timu hiyo kutolewa na mahasimu, Simba SC katika Nusu Fainali ya Kombe la Mapinduzi Jumanne usiku kwa penalti 4-2 baada ya sare ya 0-0. 
  Kipa wa Yanga, Deogratius Munishi ‘Dida’ aliokoa mkwaju wa beki Mzimbabwe Method Mwanjali wakati waliofunga penalti za timu hiyo ni Simon Msuva na kiungo Mzimbabwe, Thabani Kamusoko.
  Kipa Mghana wa Wekundu wa Msimbazi, Daniel Agyei aliokoa penalti za Dida na Mwinyi Hajji Mngwali na yeye mwenyewe kufunga penalti ya pili ya Wekundu wa Msimbazi, wakati Nahodha Jonas Mkude, Muzamil Yassin na beki Mkongo Janvier Besala Bokungu walifunga pia penalti za Simba.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA YASEMA HAINA MPANGO WA KUACHANA NA LWANDAMINA Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top