• HABARI MPYA

  Saturday, January 14, 2017

  YANGA YAENDA SONGEA BILA NGOMA, CHIRWA, ZULU

  Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
  YANGA SC itaondoka kesho kwenda Songea tayari kwa mchezo wake wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara Jumanne Uwanja wa Maji Maji Songea, lakini Mzimbabwe Donald Ngoma na Wazambia Justin Zulu na Obrey Chirwa ni kati ya wachezaji saba ambao hawatakuwamo safarini.
  Katibu wa Yanga, Baraka Deusdedit aliiambia Bin Zubeiry Sports - Online jana kwamba watatu hao wote bado ni majeruhi na wanaendelea na matibabu.
  Baraka alisema kwamba winga Emmanuel Martin yeye hatakuwamo safarini kwa sababu yuko kwenye msiba wa mdogo wake Tanga, Vincent Bossou yupo timu yake ya taifa, Togo kwenye Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) nchini Gabon, wakati mshambuliaji Malimi Busungu anaachwa kwa sababu hayupo fiti. 
  Kocha Mzambia, George Lwandamina atakwenda na kikosi cha wachezaji 20 tu kwenye mchezo huo kikiongozwa na makipa; Deo Munishi ‘Dida’ na Benno Kakolanya, mabeki Hassan Kessy, Juma Abdul, Mwinyi Mngwali, Oscar Joshua, Andrew Vincent ‘Dante’, Pato Ngonyani, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ na Kevin Yondan.
  Viungo ni Said Juma ‘Makapu’, Thabani Kamusoko, Haruna Niyonzima, Juma Mahadhi, Deus Kaseke, Simon Msuva, Yussuf Mhilu, Geoffrey Mwashiuya na washambuliaji Amissi Tambwe na Matheo Anthony. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA YAENDA SONGEA BILA NGOMA, CHIRWA, ZULU Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top