• HABARI MPYA

    Saturday, January 21, 2017

    YANGA WAITANDIKA 4-1 ASHANTI NA KUITUPA NJE ASFC

    Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
    MABINGWA watetezi, Yanga SC wamefanikiwa kwenda hatua ya 16 Bora ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Kombe la Azam Sports Federation Cup (ASFC) baada ya kuitoa Ashanti United kwa mabao 4-1 leo Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam. 
    Hadi mapumziko, Yanga walikuwa mbele kwa mabao 2-0 yaliyofungwa na wachezaji wake nyota wa kigeni, Mrundi Amissi Tambwe na Mzimbabwe, Thabani Kamusoko.
    Mshambuliaji wa zamani wa Simba, Tambwe aliwainua vitini mashabiki wa Yanga dakika ya 19 kwa shuti la karibu na lango akimalizia krosi ya winga Simon Msuva. 
    Amissi Tambwe (kulia) akipongezana na Simon Msuva baadda ya wote kufunga katika mchezo wa leo
    Amissi Tambwe akimiliki mpira mbele ya mchezaji wa Ashanti, Selemani Sultan
    Simon Msuva (kulia) akikosa bao la wazi baada ya kumdakisha kipa wa Ashanti, Rajab Kaumbu 

    aAshanti zamani ikijulikana kama Liverpool, ilikaribia kusawazisha dakika ya 25 kama si mchezaji wake, Rajab Mohammed kupiga nje.
    Kuona hivyo Yanga wakaongeza kasi ya mashambulizi na kufanikiwa kupata bao la pili dakika ya 36, mfungaji Thabani Kamusoko baada ya kuuzuia mpira ulioletwa na Ashanti na kufumua shuti lililomshinda kipa Rajab Kaumbu.
    Dakika saba tu baada ya kuanza kipindi cha pili, Yanga walifanikiwa kupata bao la pili lililofungwa na Msuva kwa penalti baada ya beki wa Ashanti, Suleiman Sultan kumuangvusha kinara huyo wa mabao wa Jangwani.
    Ashanti ikafanikiwa kupata bao la kufutia machozi dakika ya 62 kupitia kwa Isasc Hassan aliyeunganisha krosi ya Sharif Mohammed 
    Kiungo aliyepandishwa kutoka kikosi cha pili, Yussuf Mhilu akaifungia Yanga bao la nne dakika ya 89 akimalizia pasi ya Emmanuel Martin baada ya kuingia kuchukua nafasi ya Msuva.
    Kwa ujumla Yanga iliwazidi uwezo Ashanti wanaopambana katika Ligi Daraja la Kwanza Tanzania Bara na walistahili ushindi huo.
    Kikosi cha Yanga kilikuwa; Beno Kakolanya, Juma Abdul, Mwinyi Mngwali, Oscar Joshua, Andrew Vincent, Simon Msuva/Yussuf Mhilu dk82, Said Juma ‘Makapu’, Juma Mahadhi/Matheo Anthony dk78, Amissi Tambwe/Emmanuel Martin dk68 na Deus Kaseke.
    Ashanti United; Rajab Kaumbu, Hussein Mkongo, Selemani Sultan, Patrick James, Peter Mutambuzi, Zam Kuffor, Abeid Kisiga, Sharif Mohammed, Isaac Hassan, Yahya Zaidi na Rajab Mohammed.  
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: YANGA WAITANDIKA 4-1 ASHANTI NA KUITUPA NJE ASFC Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top