• HABARI MPYA

  Sunday, January 15, 2017

  WENGI WAMLILIA AMINA ATHUMANI, MWILI WAKE WAREJESHWA DAR

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  WADAU, vyama, Mashirikisho na klabu mbalimbali za michezo Tanzania zimeupokea kwa mshituko na masikitiko msiba wa Mwandishi wa Habari wa kampuni ya Uhuru Pablication, Amina Athumani.
  Amina, mwandishi wa magazeti ya Uhuru, Mzalendo na Burudani amefariki dunia usiku wa kuamkia leo katika hospitali ya Mnazi Mmoja, Zanzibar alikokuwa amelazwa kwa matibabu.
  "Amina licha ya kuwa mwandishi wa habari za michezo lakini pia alikuwa mwanachama wa Yanga tawi la Whatsapp Supportes makao makuu. Uongozi unaungana na familia ya marehemu, ndugu jamaa pamoja na tasnia nzima ya waandishi wa habari nchini katika kuomboleza kifo chake,"imesema taarifa ya Yanga.
  Uongozi wa Kampuni ya Uhuru Publications Limited, umesema kwamba Amina alilazwa kwenye hospitali hiyo baada ya kuzidiwa kutokana na kushikwa uchungu, ambapo alijifungua mtoto wa kiume, lakini kwa bahati mbaya alifariki.
  Baada ya mtoto kufariki, Amina aliendelea kupatiwa matibabu hadi mauti yalipomkumba leo asubuhi.
  Marehemu Amina alikwenda Zanzibar kikazi kwa ajili ya kuripoti mashindano ya Kombe la Mapinduzi, yaliyomalizika Ijumaa iliyopita. Ilikuwa arejee Dar es Salaam jana.
  Mipango inafanywa na ofisi kwa ajili ya kuurejesha mwili wake Dar es Salaam leo jioni kwa boti na msiba upo nyumbani kwa ndugu wa marehemu, Kariakoo.
  Mungu ilaze roho ya marehemu Amina Athumani mahala pema. Amina
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: WENGI WAMLILIA AMINA ATHUMANI, MWILI WAKE WAREJESHWA DAR Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top