• HABARI MPYA

  Saturday, January 14, 2017

  WAKATA UMEME WA AZAM, YANGA WASAINI MIAKA MIWILI OMAN

  Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
  WACHEZAJI wa zamani wa Yanga na Azam, Kipre Michael Balou na Mbuyu Junior Twite leo wamesaini mikataba ya miaka miwili kila mmoja kujiunga na klabu ya Fanja ya Oman.
  Twite raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) anayetokea Yanga na Balou raia wa Ivory Coast anayetokea Azam, wote wanahamia Oman baada ya kucheza Tanzania kwa miaka minne.
  “Leo nimesaini mkataba wa miaka miwili kujiunga na Fanja. Kukamilika kwa mpango huu ni mwanzo mpya kwangu. Naelekeza fikra zangu katika kukabiliana na changamoto mpya hapa,”alisema Balou.
  Mbuyu Twite (katikati) akikabidhiwa jezi ya Fanja baada ya kusaini mkataba wa miaka miwili leo
  Kipre Michael Balou akikabidhiwa jezi ya Fanja baada ya kusaini mkataba wa miaka miwili leo 

  Kwa upande wake, Twite alisema; “Bado nina uwezo wa kucheza mpira kwa muda mrefu tu, sina wasiwasi nitamudu changamoto za Oman na kufurahia mafanikio kama nchi nyingine nilizocheza awali,”.
  Wakati kwa Balou hii ni nchi ya pili kwake kucheza nje ya nyumbani baada ya Tanzania, kwa Twite Oman ni nchi ya tatu kucheza nje ya DRC baada ya Rwanda alikochezea APR na Tanzania Yanga.
  Na wote wawili wana sifa zinazofanana, wanaweza kucheza kama mabeki wa pembeni na pia kama viungo wa kati, hususan wa ulinzi – uwezo ambao waliuthibitisha walipokuwa wanacheza Ligi ya Tanzania.
  Balou anakwenda Oman baada ya pacha wake wa kuzaliwa, Kipre Herman Tchetche waliyekuwa naye Azam FC kwa kipindo chote hicho, kutangulia huko akijiunga na Al Suwaiq.
  Twite na Balou katika klabu ya Fanja wanaungana na mchezaji mwingine aliyekuwa anacheza Tanzania, Danny Lyanga aliyewika Simba SC ya Dar es Salaam na Coastal Union ya Tanga.     
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: WAKATA UMEME WA AZAM, YANGA WASAINI MIAKA MIWILI OMAN Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top