• HABARI MPYA

  Tuesday, January 10, 2017

  VIKOSI VYA LEO SIMBA NA YANGA; TAMBWE, LUIZIO WANAAANZA, NGOMA MAVUGO NJE

  Na Mwandishi Wetu, ZANZIBAR
  YANGA itawakosa mshambuliaji wake hatari Mzimbabwe Donald Dombo Ngoma katika mchezo wa Nusu Fainali ya Kombe la Mapinduzi usiku huu Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
  Pamoja na Ngoma, Yanga itawakosa viungo Wazambia Justin Zulu na Obrey ambao kwa pamoja na Ngoma ni majeruhi.
  Kwa sababu hiyo, kocha Mzambia George Lwandamina ameanza na mshambuliaji mmoja tu halisi, Mrundi Amissi Tambwe ambaye naye analazimishwa kucheza akiwa na maumivu. 
  Upande wa Simba, kocha Mcameroon, Joseph Omog amemuanzishia nje mshambuliaji Mrundi, Laudit Mavugo aliyefunga mabao yote katika ushindi wa 2-0 dhidi ya Jang'ombe Boys kwenye Nusu Fainali. 
  Kikosi cha Yanga SC leo kipo hivi; Deogratius Munishi ‘Dida’, Juma Abdul, Mwinyi Hajji, Andrew Vincent ‘Dante’, Kelvin Yondan, Saidi Juma ‘Makapu’, Simoni Msuva, Thabani Kamusoko, Amissi Tambwe, Haruna Niyonzima na Deusi Kaseke. 
  Simba SC; ⁠⁠Daniel Agyei, Janvier Bokungu, MOhammed Hussein 'Tshabalala', Abdi Banda, Method Mwanjali, Jonas Mkude, Shiza Kichuya, James Kotei, Juma Luizio, Muzamil Yassin na Mohamed Ibrahim.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: VIKOSI VYA LEO SIMBA NA YANGA; TAMBWE, LUIZIO WANAAANZA, NGOMA MAVUGO NJE Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top