• HABARI MPYA

    Monday, January 02, 2017

    TFF YAACHANA NA MKWASA, MAYANGA KOCHA MPYA STARS

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    RAIS wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi amemtangaza Salum Mayanga kuwa kocha mpya wa muda wa timu ya taifa, Taifa Stars.
    Malinzi amesema leo kwamba hiyo inafuatia aliyekuwa kocha wa Taifa Stars, Charles Boniface Mkwasa kumaliza Mkataba wake leo.
    Majukumu ya Mayanga yatakuwa ni kuandaa kikosi cha Taifa Stars kwa ajili ya mechi za kufuzu Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2019 ambazo mechi za awali zitanza mapema mwaka huu.
    Mayanga atakuwa na jukumu la kuandaa kikosi cha wachezaji wa ndani kwa ajili ya mechi za kufuzu CHAN.
    TFF inamshukuru Kocha Charles Boniface Mkwasa kwa utumishi katika nafasi hiyo ulioanza Julai, 2015 akimrithi Mholanzi, Mart Nooij na kumtakia mafanikio katika mipango yake inayofuata.
    Katika kipindi chake cha kuwa Taifa Stars, Mkwasa ameiongoza timu katika mechi 13, ikishinda mbili, kufungwa sita na sare tano.

    Chini ya Charles Boniface Mkwasa (kulia) Taifa Stars, imeshinda mechi mbili tu kati ya 13, ikifungwa sita na sare tano

    REKODI YA MKWASA TAIFA STARS
    Tanzania 1-1 Uganda (Kufuzu CHAN, Kampala)
    Tanzania 1-2 Libya (Kirafiki Uturuki)
    Tanzania 0-0 Nigeria (Kufuzu AFCON Dar)
    Tanzania 2-0 Malawi (Kufuzu Kombe la Dunia Dar)
    Tanzania 0-1 Malawi (Kufuzu Kombe la Dunia Blantyre)
    Tanzania 0-2 Afrika Kusini U23 (Kirafiki Johannesburg)
    Tanzania 2-2 Afrika Kusini U23 (Kufuzu Kombe la Dunia Dar)
    Tanzania 2-2 Afrika Kusini U23 (Kufuzu Kombe la Dunia Dar)
    Algeria 7-0 Tanzania (Kufuzu kombe la Dunia Blida)
    Tanzania 1-0 Chad (Kufuzu AFCON D’jamena)
    Tanzania 0-2 Misri (Kufuzu AFCON Taifa)
    Tanzania 1-1 Kenya (Kirafiki Nairobi)
    Tanzania 0-3 Zimbabwe (Kirafiki Harare)
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: TFF YAACHANA NA MKWASA, MAYANGA KOCHA MPYA STARS Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top