• HABARI MPYA

    Tuesday, January 03, 2017

    SIMBA YATINGA NUSU FAINALI KOMBE LA MAPINDUZI

    Na Mwandishi Wetu, ZANZIBAR
    SIMBA SC imekwenda Nusu Fainali ya Kombe la Mapinduzi baada ya ushindi wa bao 1-0 dhidi ya KVZ usiku huu Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
    Ushindi huo uliotokana na bao pekee la kiungo Muzamil Yassin dakika ya 43, unaifanya Simba SC ifikishe pointi sita baada ya kucheza mechi mbili.
    Sifa zaidi zimuendee beki Abdi Hassan Banda aliyeyafanikiwa kuvunja mtego wa kuotea wa KVZ ma kumchomea pasi nzuri Muzamil aliyekwenda kufunga.
    Huu unakuwa ushindi wa pili mfululizo kwa Simba katika michuano hii, baada ya juzi kuilaza Taifa Jang’ombe 2-1.
    KVZ ilimaliza pungufu mchezo huo baada ya beki wake, Rashid Omar Rashid kutolewa kwa kadi nyekundu kufuatia kumkwatua mshambuliaji wa Simba, Pastory Athanas nje kidogo ya boksi akiwa anakwenda kufunga. 
    Katika mchezo wa Kundi A uliotangulia leo, Jang’ombe Boys iliwalaza mabingwa watetezi, URA ya Uganda 2-1.
    Michuano hiyo itaendelea kesho kwa mechi za Kundi B, kati ya Zimamoto na Yanga kuanzia Saa 10:00 jioni na Jamhuri dhidi ya Azam kuanzia Saa 2:30 usiku.
    Kikosi cha Simba leo kilikuwa; Daniel Agyei, Janvier Besala Bokungu, Mohamed Hussein ‘Tshabalala’, Method Mwanjali, Abdi Banda, Jonas Mkude, Shiza Kichuya, James Kotei, Athanas Pastory, Juma Luizio na Muzamil Yassin.
    KVZ; Abdallah Bakari, Saleh Nassor, Makarani Mluchu, Rashid Omar, Said Mohammed, Suleiman Ali, Suleiman Hassan, Suleiman Juma, Sultan Kasikasi, Mohammed Maulid na Masoud Abdllah.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SIMBA YATINGA NUSU FAINALI KOMBE LA MAPINDUZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top