• HABARI MPYA

    Monday, January 09, 2017

    SIMBA NA YANGA NNE ZILIZOPITA KWENYE ARDHI YA ZANZIBAR...

    Na Haji Manara, ZANZIBAR
    KESHO Jumane usiku pale Amaan Stadium patachezwa mechi ya nusu fainali ya kombe la Mapinduzi baina ya klabu kongwe zaid kwenye ukanda huu wa Africa Mashariki, Simba na Yanga. 
    Ni mechi ya tano kwa miamba hiyo ya soka kukutana kwenye uwanja huo wenye historia pana sio Zanzibar tu, bali hata Tanzania kwa ujumla. 
    Mara ya kwanza klabu hizi zilikutana mwaka 1975 kwenye fainali ya klabu bingwa Afrika mashariki na kati, ambapo Yanga ilishinda kwa goli mbili kwa bila, magoli yakifungwa na marehemu Gibson Sembuli na baba yangu Al Haji Sunday Ramadhan Manara Computer, ni mechi iliokuwa kali na nilijuzwa ndio asili ya kumeguka kwa Simba na kuundwa klabu ya Nyota Nyekundu. 
    Zama hizo babu yangu mzaa mama marhumu Hassan Haji alikuwa mwenyekiti wa Simba, na wanachama wa Simba wakahoji ktk mkutano mkuu kwa nn Sunday atufunge kila siku au kwa kuwa ni mkwe wa Mwenyekiti? Taarifa ya maneno hayo yaliibua sintofahamu kubwa klabuni, hali iliopelekea wanachama waasisi wa klabu(waswahili kwenda kuanzisha klabu yao ya Red Star. 
    Ikumbukwe game ya Zbar ilichezwa muda mfupi baada ya fainali ya ligi ya taifa pale Nyamagana Stadium Mwanza, ambapo Yanga ilifungwa na  Simba 2-1, kwa magoli ya Sunday na Sembuli,  
    Moja ya jambo lingine la kukumbukwa kwenye mchezo huu ni kuzaliwa kwa mwandishi wa makala hii siku Yanga ikicheza na Mufurila Wonderess kwenye nusu fainali ya kombe hilo, ambalo Simba ndio timu ya kwanza kulitwaa na Bingwa wa kihistoria wa muda wote wa ukanda huu murua.
    Mechi ya pili miamba hii kukutana ilikuwa pia ktk fainali ya kombe hili, na Simba kulipa kisasi kwa kuifunga Yanga kwa mikwaju ya Penati 6-5, huku mkwaju wa mwisho ukikoswa na beki wa Yanga, David Mwakalebela, Mungu alinijaalia kuishuhudia mechi hii kabambe mno pale Zbar, nikishuhudia ufundi wa hali ya juu katikati ya uwanja,baina ya Hussen Masha, Michael Paul, Ramadhani Lenny kwa upande wa Simba, na Issa Athman, Method Mogella, Steven Mussa na Hamis Gaga kwa upande wa Yanga.
    Kwangu hii ilikuwa mechi bora kuwahi kuishuhudia baina ya watani hao, ikumbukwe dakika 120 zilishuhudia sare ya 1-1, huku Simba ikitangulia kwa goli la Hussen Masha na Yanga wakisawazisha kwa goli la Said Mwamba kizota, nikujuze pia jina la Taifa kubwa ndio lilipobamba wakati wa michuano hii mikubwa zaid kwa ngazi ya vilabu kwenye eneo hili la Afrika. 
    Mwaka huo huo 1992 tulishuhudia nusu fainali ya kombe la Muungano baina ya timu hz, ukiwa ni mchezo wa tatu baina yao kuchezwa visiwani Zbar, mchezo huu Simba pia ilishinda goli moja kwa Sifuri, goli safi la mwalimu wa lugha ktk shule ya kimataifa nchini na Mrundi wa Kibaha, Daniel kimti, hii ndio game ya mwisho ktk utawala wa Mikidadi kassanda kama mwenyekiti wa Simba na baada ya hapo Marehemu Amiri Ally Bamchawi akawa Mwenyekiti wa Simba,
    Kumbuka Bamchawi alikuwa meneja wa timu wakati wa mgogoro wa 1975, lakini baadae alirudi Simba hadi mauti yalipomkuta. 
    Mechi ya nne na ya mwisho kuwakutanisha Simba na Yanga zbar ni januari 2011, kwenye kombe hili la Mapinduzi na ilikuwa ni mchezo wa fainali ambapo Simba Iliendeleza umwamba wake kwa kuitandika Yanga 2-0,magoli ya Shija Mkina na Mussa Hassan Mgosi, Meneja wa sasa wa kikosi cha Simba.
    Nimekupeni historia hii murua vjana wa dotcom ili mpate kujua tulipotoka, mategemeo yetu pia kwa kesho,waamuzi watazingatia sheria 17 za soka. 
    Tukutane kesho Amaan Stadium tukimkomala Nyani usoni. 
    Mwana kulitaka, Mwana kulipewa.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SIMBA NA YANGA NNE ZILIZOPITA KWENYE ARDHI YA ZANZIBAR... Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top