• HABARI MPYA

    Thursday, January 05, 2017

    SIMBA NA URA HAKUNA MBABE, SARE 0-0

    Na Mwandishi Wetu, ZANZIBAR
    MABINGWA watetezi, URA ya Uganda wamelazimishwa sare ya 0-0 na Simba SC katika mchezo wa Kundi A Kombe la Mapinduzi usiku huu Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
    Kwa sare hiyo, URA inafikisha pointi nne na italazimika kushinda mchezo wa mwisho Jumapili na Taifa Jang’ombe ili kwenda Nusu Fainali.
    Simba SC wao wanafikisha pointi saba na kuzidi kujiongezea matumaini ya kwenda Nusu Fainali.
    Kipa Peter Manyika alianzishwa leo baada ya muda mrefu na kudaka vizuri.
    Kocha Mcameroon, Joseph Marius Omog aliwaanzisha washambuliaji wawili Mrundi Laudit Mavugo na mzawa Juma Luizio, huku pembeni wakicheza Shizza Kichuya na Pastory Athanas lakini wakashindwa kumpa hata bao moja. 
    Lakini mchezo ulikuwa mzuri na mashambulizi yalikuwa ya pande zote mbili.
    Kikosi cha Simba kilikuwa; Peter  Manyika, Janvier Bokungu, Mohammed  Hussein ‘Tshabalala’,  Abdi  Banda, Method  Mwanjali,  Shiza Kichuya/Hijja Ugando dk87, Muzamil Yassin,  Juma Luizio, Laudit Mavugo/Jamal Mnyate dk80 na  Pastory Athanas. 
    URA: Alionzi Nafian, Kulaba Jimmy,  Sekito Sam, Mumaba Allan, Ntambi Julius, Muliky Hudu/Elkanah Nkugwa dk74, Lule Jimmy, Bekota Labama, Kigongo Renald/Makogotya Robert dk54 na Kagimu Shafiq.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SIMBA NA URA HAKUNA MBABE, SARE 0-0 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top