• HABARI MPYA

  Thursday, January 12, 2017

  SIMBA HAITAKI KUWAFIKISHA AZAM KWENYE MATUTA, YATAKA KUWAMALIZA MAPEMAAA

  Na Mwandishi Wetu, ZANZIBAR
  KOCHA Msaidizi wa Simba, Mganda Jackson Mayanja amesema kwamba hawataki kufikishana kwenye penalti na Azam kesho usiku katika fainali ya Kombe la Mapinduzi Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
  Mayanja aliyekuwa anazungumza kwa niaba ya bosi wake, Mcameroon Joseph Marius Omog alisema kwamba mchezo wa kesho dhidi ya Azam utakuwa mgumu, lakini watajitahidi kuumaliza mapema.
  Baada ya kuwatoa mahasimu, Yanga kwa penalti 4-2 kufuatia sare ya 0-0 ndani ya dakika 90 Uwanja wa Amaan, Zanzibar juzi – kesho Simba itamenyana na Azam katika fainali. 
  “Azam walishinda katika mchezo wa kukumbukwa dhidi ya Yanga 4-0 kabla ya kwenda kuwatoa Taifa Jang’ombe katika Nusu Fainali (1-0). na sasa wanakutana na timu nyingine bora, Simba. Utakuwa mchezo mzuri,”alisema.
  Simba itakuwa na matayarisho yake ya mwisho leo kabla ya mchezo huo unaosubiriwa kwa hamu na mashabiki wa soka kote nchini.
  Katika mechi na Yanga, penalti za Simba zilifungwa na Nahodha Jonas Mkude, kipa Daniel Agyei, Muzamil Yassin na beki Mkongo Janvier Besala Bokungu. Kipa wa Yanga, Deogratius Munishi ‘Dida’ aliokoa mkwaju wa beki Mzimbabwe Method Mwanjali wakati waliofunga penalti za timu hiyo ni Simon Msuva na kiungo Mzimbabwe, Thabani Kamusoko wakati kipa Mghana wa Wekundu wa Msimbazi, Daniel Agyei aliokoa penalti za Dida na Mwinyi Hajji Mngwali.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA HAITAKI KUWAFIKISHA AZAM KWENYE MATUTA, YATAKA KUWAMALIZA MAPEMAAA Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top