• HABARI MPYA

  Wednesday, January 18, 2017

  SAMATTA AKIPIGA MWANZO MWISHO, GENK YAPATA SARE UGENINI

  Na Mwandishi Wetu, GENK
  MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta Jumanne amecheza kwa dakika zote 90 timu yake, KRC Genk ikilazimisha sare ya 1-1 ugenini na KV Oostende katika mchezo wa Kombe la Ubelgiji Uwanja wa Versluys Arena, Oostende.
  Katika mchezo huo, wenyeji walitangulia kwa bao la kiungo Mfaransa, Kevin Vandendriessche dakika ya 21, kabla ya kiungo wa Ukraine, Ruslan Malinovskiy kuisawazishia Genk dakika ya 55.
  Leo Samatta amecheza mechi ya 37 Genk,18 msimu uliopita na 19 msimu huu na kati ya hizo, ni michezo 18 tu ndiyo alianza, 10 msimu uliopita na saba msimu huu.
  Mbwana Samatta akimiliki mpira mbele ya beki wa KV Oostende Jumanne

  Mechi 19 kati ya hizo alitokea benchi, nane msimu uliopita na 11 msimu huu, wakati nane hakumaliza baada ya kutolewa, sita msimu uliopita na mbili msimu huu huku akiwa amefunga jumla ya mabao tisa, manne msimu huu na matano msimu uliopita.
  Kikosi cha KRC Genk kilikuwa: Bizot, Uronen, Colley, Dewaest, Castagne, Heynen, Pozuelo/Berge dk92 Malinovskyi/Kumordzi dk85, Trossard/Buffalo dk62, Bailey na Samatta.
  Drawing KV Oostende : Dutoit, Capon, Rozehnal, Milic, Marusic, Jonckheere, Vandendriessche, Berrier/Cyriac dk79 Canesin/Conte dk72, El Ghanassy na Dimata/Jali dk87.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SAMATTA AKIPIGA MWANZO MWISHO, GENK YAPATA SARE UGENINI Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top