• HABARI MPYA

  Monday, January 09, 2017

  RONALDO AMBWAGA TENA MESSI, ASHINDA TUZO YA MWANASOKA BORA WA FIFA

  MSHAMBULIAJI Cristiano Ronaldo ameshinda tuzo ya Mchezaji Bora wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) mwaka 2016 baada ya kutwaa taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya na Real Madrid na kuiwezesha Ureno kutwaa Kombe la Euro.
  Nyota huyo mwenye umri wa miaka 31 kwa mara nyingine amemuangusha mpinzani wake, Lionel Messi kama alivyofanya awali mwezi uliopita kwenye Ballon d'Or. 
  Messi, ambaye hakuhudhuria sherehe hizo mjini Zurich, Uswisi kutokana na majukumu yake Barcelona, na mshambuliaji wa Atletico Madrid, Antoine Griezmann wote waliangushwa na mshambuliaji huyo wa Ureno.
  Nyota wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo akikabidhiwa tuzo yake na Rais wa FIFA, Gianni Infantino jana mjini Zurich PICHA ZAIDI GONGA HAPA 

  Akizungumza baada ya kushinda tuzo hiyo mjini Zurich, Ronaldo alisema: "Kama nilivyowahi kusema mara nyingi, mwaka jana ulikuwa mwaka wa ndoto. Real Madrid ilishinda Ligi ya Mabingwa, na Ureno ubingwa wa Ulaya. Ninajivunia na nina furaha sana, na ninawashukuru wachezaji wenzangu kwa mwaka mzuri,"alisema.
  Wakati huo huo; Ronaldo kwa mara ya kwanza aliibuka na mpenzi wake mpya, Georgina Rodriguez baada ya tetesi za kwamba wapo kwenye mahusiano. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: RONALDO AMBWAGA TENA MESSI, ASHINDA TUZO YA MWANASOKA BORA WA FIFA Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top