• HABARI MPYA

  Sunday, January 08, 2017

  PAMOJA NA KULA 4-0 YANGA BADO WABABE WA AZAM FC

  Na Mwandishi Wetu, ZANZIBAR
  UPINZANI wa Azam na Yanga katika soka jana umechukua hatua mpya baada ya kukutana katika mechi ya mwisho ya Kundi B Kombe la Mapinduzi.
  Katika mchezo huo uliofanyika Uwanja wa Amaan, Zanzibar Azam iliichapa Yanga mabao 4-0 na kufanya timu zote zimalize na pointi saba baada ya kushinda mechi mbili na sare moja.
  Azam anamaliza kileleni mwa kundi kutokana na wastani wake mzuri wa mabao, akifuatiwa na Yanga na timu zote zinakwenda Nusu Fainali kukutana na timu za Kundi A. 
  Mabao ya Azam jana yalifungwa na John Raphael Bocco dakika ya pili, Yahya Mohammed dakika ya 54, Joseph Mahundi dakika ya 80 na 
  Enock Atta Agyei dakika ya 85.
  Huo ulikuwa mchezo wa 27 kihistoria kuzikutanisha timu hizo kwenye mashindano mbalimbali, kati ya hizo Yanga ikishinda 10, Azam tisa na nane wametoka sare.   

  REKODI YA YANGA NA AZAM FC: 
                      P     W   D   L   GF   GA   GD Pts
  Yanga SC    27   10   8   9   35   34     1     38
  Azam FC     27   9     8   10   34   35    -1     35

  MECHI ZILIZOPITA ZA AZAM NA YANGA:
  Janauri 7, 2017
  Azam 4-0 Yanga (Kombe la Mapinduzi Zanzibar)
  Oktoba 16, 2016
  Yanga 0-0 Azam (Ligi Kuu Uhuru)
  Agosti 17, 2016
  Azam FC 2-2 Yanga SC (Ngao; Penalti 4-1 Taifa)
  Mei 25, 2016
  Yanga 3-1 Azam FC (Fainali Kombe la ASFC)
  Machi 5, 2016 
  Yanga 2-2 Azam FC (Ligi Kuu Taifa)
  Januari 5, 2016 
  Yanga SC 1-1 Azam (Kombe la Mapinduzi)
  Oktoba 17, 2015 
  Yanga SC 1-1 Azam (Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara)
  Agosti 22, 2015
  Yanga 0-0 Azam FC (Yanga ilishinda kwa penalti 8-7 Ngao ya Jamii)
  Julai 29, 2015
  Azam 0-0 Yanga SC (Azam ilishinda kwa penalti 5-3 Robo Fainali Kombe la Kagame)
  Mei 6, 2015
  Azam 2-1 Yanga SC (Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara)
  Desemba 28, 2014
  Yanga SC 2-2 Azam (Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara)
  Septemba 14, 2014
  Yanga SC 3-0 Azam FC (Ngao ya Jamii)
  Machi 19, 2014; 
  Yanga SC 1-1 Azam FC (Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara)
  Septemba 22, 2013; 
  Azam FC 3-2 Yanga SC (Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara)
  2013: Yanga SC 1-0 Azam FC
  Februari 23, 2013;  
  Yanga SC 1-0 Azam FC (Ligi Kuu Taifa)
  Novemba 4, 2012;  
  Azam FC 0-2 Yanga SC (Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara)
  Julai 28, 2012
  Yanga 2-0 Azam (Fainali Kombe la Kagame Taifa)
  Machi 10, 2012; 
  Yanga SC 1-3 Azam FC (Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara)
  January 07, 2012
  Azam FC 3-0 Yanga SC (Robo Fainali Kombe la Mapinduzi)
  Septemba 18, 2011;  
  Azam 1-0 Yanga SC (Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara)
  Machi 30, 2011;  
  Yanga SC 2-1 Azam FC (Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara)
  Desemba 20, 2011
  Azam 2-1 Yanga (Mechi ya Hisani; Kuchangia Walemavu Taifa)
  Oktoba 24, 2010; 
  Azam FC 0-0 Yanga SC (Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara)
  Machi 7, 2010;  
  Yanga SC 2-1 Azam FC (Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara)
  Oktoba 17, 2009; 
  Azam FC 1-1 Yanga SC (Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara)
  Aprili 8, 2009;  
  Yanga SC 2-3 Azam FC (Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara)
  Oktoba 15, 2008;  
  Azam FC 1-3 Yanga SC (Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara)
  (Rekodi hii inahusisha mechi zote za mashindano maalum, ambayo timu hizo zimekutana)
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: PAMOJA NA KULA 4-0 YANGA BADO WABABE WA AZAM FC Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top