• HABARI MPYA

    Thursday, January 12, 2017

    NGASSA: YANGA INAKOSA WACHEZAJI WAWILI MUHIMU SANA

    Na Mwandishi Wetu, MBEYA
    KIUNGO wa kimataifa wa Tanzania, Mrisho Khalfan Ngassa amesema kwamba Yanga inahitaji wachezaji wawili wa kuchezesha timu ili kuwa na uwiano mzuri kikosini.
    Ngassa ambaye kwa sasa anachezea Mbeya City, alisema leo katika mahojiano na Bin Zubeiry Sports - Online kwamba Yanga inahitaji wachezaji wenye uwezo mkubwa wa kuuchezea mpira na kutoa pasi za mwisho.    
    “Ukiangalia Yanga wanavyocheza kwa sasa, unaona kabisa inakoa watu kama wawili wa kuchezea mpira na kutoa pasi za mwisho kama alivyo Niyonzima (Haruna). Ili wawe na uwiano mzuri katika timu, lazima wawapete hao watu,”alisema.
    Mrisho Ngassa amesema Yanga inakosa wachezaji wawili muhimu kikosini mwake 

    Maoni hayo ya Ngassa yanafuatia Yanga kufanya vibaya katika michuano ya Kombe la Mapinduzi wakitolewa na Simba SC kwa penalti 4-2 Jumanne usiku Uwanja wa Amaan, Zanzibat baada ya sare ya 0-0 ndani ya dakika 90.  
    “Mechi ilikuwa nzuri, Simba waliwazidi katikati Yanga, ambao walikuwa wanacheza mipira mirefu kumtumia Msuva (Simon) peke yake, hivyo Simba wakagundua njia hiyo, baada ya kusogea pembeni mipango wakauwa,”alisema.
    Pamoja na hayo, Ngassa alisema kwamba wachezaji wengi wa Yanga kwa sasa wamechoka baada kucheza mashindano mengi mfululizo msimu uliopita, hivyo wengi wao miili yao imechoka.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: NGASSA: YANGA INAKOSA WACHEZAJI WAWILI MUHIMU SANA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top