• HABARI MPYA

    Sunday, January 15, 2017

    MWANDISHI AFARIKI DUNIA BAADA YA KURIPOTI KOMBE LA MAPINDUZI MWANZO MWISHO

    Na Mwandishi Wetu, ZANZIBAR
    MWANDISHI wa Habari za michezo wa magazeti ya Uhuru, Mzalendo na Burudani, Amina Athumani amefariki dunia usiku wa kuamkia leo katika hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar.
    Amina alikuwa visiwani Zanzibar kikazi, kuripoti michuano ya Kombe la Mapinduzi na Mwenyezi Mungu akamuongoza kuifanya kazi yake vizuri mwanzo hadi mwisho.
    Usiku wa kuamkia safari ya kurejea Dar es Salaam Jumamosi ndipo Amina aliyekuwa ana uja uzito wa miezi saba alipoanza kusumbuliwa kiafya.
    Amina Athumani amefariki dunia usiku wa kuamkia leo katika hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar

    Na inaelezwa asubuhi wakati anaelekea kwenye boti kurejea Dar es Salaam alianguka na kupelekwa hospitali binafsi, baadaye akahamishiwa Mnazi Mmoja. Siku hiyo hiyo Amina akajifungua mtoto ambaye kwa bahati mbaya alikwishafariki dunia.
    Na usiku wa kuamkia leo naye amefariki pia. Taarifa zaidi za msiba huo zinatarajiwa baadaye kutoka kwa wahusika, hususan familia ya marehemu na waajiri wake, Uhuru Publication Limited. Mungu ampumzishe kwa amani Amina Athumani.   
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MWANDISHI AFARIKI DUNIA BAADA YA KURIPOTI KOMBE LA MAPINDUZI MWANZO MWISHO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top