• HABARI MPYA

  Thursday, January 05, 2017

  MPINZANI WA NAMBA WA SAMATTA AUMIA GOTI, ATAKUWA NJE MIEZI NANE

  MSHAMBULIAJI Mgiriki Nikolaos Karelis anayecheza nafasi moja na Mtanzania Mbwana Ally Samatta katika klabu ya KRC Genk ya Ubelgiji ameumia goti na atakuwa nje kwa miezi nane.
  Karelis aliumia mwishoni mwa mwaka katika mchezo dhidi ya KAA Gent Desemba 27, Uwanja wa Laminus Arena Genk ikishinda 2-0, tena yeye akifunga bao la pili dakika ya 26.
  Nikolaos Karelis anayecheza nafasi moja na Mbwana Samatta atakuwa nje kwa miezi nane

  Na baada ya kufanyiwa vipimo siku iliyofuata, ikagundulika Karelis ameumia vibaya goti la mguu wake wa kushoto na atahitaji kufanyiwa upasuaji, ambao utamuweka nje ya uwanja si chini ya miezi minane.
  Wakati Karelis akienda kwenye matibabu, KRC Genk sasa itamtegemea Samatta kwa kipindi chote hicho.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MPINZANI WA NAMBA WA SAMATTA AUMIA GOTI, ATAKUWA NJE MIEZI NANE Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top