• HABARI MPYA

  Monday, January 09, 2017

  MKUDE: MECHI NA YANGA ITAKUWA NGUMU KESHO

  Na Mwandishi Wetu, ZANZIBAR
  NAHODHA wa Simba, Jonas Mkude amesema kwamba mechi dhidi ya Yanga itakuwa ngumu kwa sababu kila timu imejiandaa vizuri.
  Akizugumza jana baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Jang’ombe Boys kwenye mchezo wa mwisho wa Kundi A, Mkude alisema kwamba hawana wasiwasi wowote kuelekea Nusu Fainali dhidi ya mahasimu, Yanga.
  “Sisi tumejiandaa vizuri, ni matumaini yetu na wao wamejiandaa vizuri, mchezo wa mpira wa miguu ni maandalizi, baada ya maandalizi tutakutana tutacheza, utakuwa mchezo mzuri, kipimo kizuri kwetu na kwao, dakika 90 zitaamua,”.
  Jonas Mkude (kushoto) amesema mechi dhidi ya Yanga itakuwa ngumu kesho

  Simba na Yanga zitakutana katika Nusu Fainali ya Pili ya Kombe la Mapinduzi kesho Saa 2:15 usiku Uwanja wa Amaan, Zanzibar.  Hiyo inafuatia Simba kumaliza kileleni mwa Kundi A kwa pointi zake 10, ikifuatiwa na Taifa Jang’ombe pointi tisa, Jang’ombe Boys pointi sita na URA pointi nne. 
  Ikumbukwe Yanga imeshika nafasi ya pili Kundi B nyuma ya Azam walioongoza kwa wastani wa mabao baada ya kufungana kwa pinti saba kila timu.
  Mabao yote ya Simba SC jana yalifungwa na mshambuliaji wa kimataifa wa Burundi, Laudit Mavugo moja kila kipindi. Nusu Fainali ya kwanza kesho itazikutanisha Azam FC na Taifa Jang’ombe Saa 10:30 jioni.
  Hiyo inafuatia Taifa kuwalaza waliokuwa mabingwa watetezi, URA ya Uganda 1-0 katika mchezo wa mwisho wa Kundi A usiku wa jana Uwanja wa Amaan.
  Bao pekee la Taifa Jang’ombe limefungwa na Mohammed Said kwa penalti, baada ya Ally Badru kuangushwa kwenye boksi. Mapema URA nao walipoteza penalti baada ya Bogota Labama kuangushwa kwene boksi.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MKUDE: MECHI NA YANGA ITAKUWA NGUMU KESHO Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top