• HABARI MPYA

  Wednesday, January 18, 2017

  MBEYA CITY YAIKOMALIA AZAM CHAMAZI, SARE 0-0

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  AZAM FC imelazimishwa sare ya 0-0 na Mbeya City katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
  Matokeo ya mchezo huo uliochezwa kuanzia Saa 1:00 usiku, yanaifanya Azam FC ifikishe pointi 31 baada ya kucheza mechi 19 na kupanda kwa nafasi moja hadi ya tatu, nyuma ya Simba yenye pointi 45 na Yanga pointi 43 za mechi 19 pia.
  Mbeya City yenyewe inafikisha pointi 25 baada ya kucheza mechi 19 na inapanda kwa nafasi moja hadi ya sita, ikiishushia nafasi ya saba Stand United yenye pointi 25 za mechi 19 pia, lakini inazidiwa wastani wa mabao. 
  Katika mchezo wa leo, kipindi cha kwanza Mbeya City walicheza kwa kujihami zaidi na kuwanyima kabisa mwanya mabingwa wa Kombe la Mapinduzi.
  Kiungo mshambuliaji wa zamani wa Azam FC, Mrisho Khalfan Ngassa aliingia zikiwa zimebaki dakika 23 na akakaribia kuifungia timu yake mpya, Mbeya City baada ya kupiga shuti lililogonga mwamba, 
  Kikosi cha Azam FC kilikuwa; Aishi Manula, Shomary Kapombe, Gardiel Michael, Aggrey Morris, Yakoub Mohammed, Stephane Kingue, Salum Abubakar ‘Sure Boy’, Himid Mao/Frank Domayo dk58, Joseph Mahundi/Shaaban Iddi dk86, Yahya Mohammed/Samuel Afful dk70 na John Bocco.
  Mbeya City; Owen Chaima, Haruna Shamte, Hassan Mwasapili, Tumba Lui/Zahor Pazi dk25, Sankan Mkandawile, William Otong, Raphael Daudi, Kenny Ally, Tito Okello/Mrisho Ngassa dk77, Ditram Nchimbi na Ayoub Semtawa.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MBEYA CITY YAIKOMALIA AZAM CHAMAZI, SARE 0-0 Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top