• HABARI MPYA

  Thursday, January 05, 2017

  MBEYA CITY WAENDA SUMBAWANGA KUIPASHIA AZAM

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  TIMU ya Mbeya City itaondoka kesho asubuhi mjini Mbeya kwenda Sumbawanga mkoani Rukwa kwa ziara ya michezo ya kirafiki. 
  Meneja wa Mbeya City, Geoffrey Katepa alisema jana mazungumzo na Bin Zubeiry Sports - Online kwamba, kikosi cha timu hiyo kitakuwa huko kwa mechi tatu za kujipima nguvu hadi wiki ijayo.
  Katepa, kiungo wa zamani wa Yanga alisema kwamba ziara inakuja baada ya mapumziko ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kupisha michuano ya Kombe la Mapinduzi visiwani Zanzibar.
  Mbeya City itaondoka kesho asubuhi mjini Mbeya kwenda Sumbawanga mkoani Rukwa kwa ziara ya michezo ya kirafiki

  “Imekuwa ni taarifa njema kupatikana kwa michezo hii ya kirafiki na tutaitumia  kujiweka sawa kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wetu wa Januari 17 dhidi ya Azam FC kule Uwanja wa Azam Complex, Chamazi mjini Dar es Salaam,” alisema Katepa.
  Katepa aliyewahi pia kuchezea Tukuyu Stars ya Mbeya, alisema kwamba Mbeya City itacheza mechi tatu kuanzia Ijumaa ya leo Ijumaa, Jumamosi na Jumapili kabla ya kurejea Mbeya Jumatatu kuendelea na maandalizi ya mechi dhidi ya Azam.
  Alisema mechi zote zitachezwa Uwanja wa Mandela na kwa mujibu wa ratiba wataanza na Magogo FC kabla ya kucheza na timu nyingine watakazopangiwa na wenyeji wao. Alisema watasafiri na kikosi cha wachezaji  25 na viongozi watano.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MBEYA CITY WAENDA SUMBAWANGA KUIPASHIA AZAM Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top