• HABARI MPYA

  Thursday, January 19, 2017

  MACHUPPA: ILI KWENDA AFCON TUJIPANGE HASWA

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  MSHAMBULIAJI wa zamani wa kimataifa wa Tanzania, Athumani Machuppa amesema si rahisi Tanzania kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka 2019 kama baadhi wanavyofikiria.
  Baada ya Taifa Stars kupangwa Kundi L kufuzu AFCON mwaka 2019 nchini Cameroon pamoja na timu za Uganda, Cape Verde na Lesotho wiki iliyopita mjini Libvreville, Gabon wengi wanaamini njia nyeupe kwenda Cameroon 2019.
  Lakini Machuppa anasema; “Kama tunataka kwenda Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka 2019 lazima tujipange haswa,”.
  Akifafanua mchezaji huyo wa zamani wa Simba, Al Hemria, Sharjah za Dubai, Atraco FC ya Rwanda, Aalborg FF ya Denmark na Vasalund IF ya Sweden, amesema kujipanga ni kwa maandalizi, kwani viwango vya wapinzani wetu katika Kundi L si vya kubeza.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MACHUPPA: ILI KWENDA AFCON TUJIPANGE HASWA Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top