• HABARI MPYA

  Sunday, January 08, 2017

  LWANDAMINA 'ABANDIKA PLASTA' MDOMONI

  Na Mwandishi Wetu, ZANZIBAR
  KOCHA wa Yanga, Mzambia George Lwandamina leo amekataa kabisa kuuzungumzia mchezo wa jana dhidi ya Azam FC. 
  Yanga ilifungwa 4-0 na Azam jana katika mchezo wa mwisho wa Kundi B Kombe la Mapinduzi Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
  Kipigo hicho kimewashitua wapenzi na wanachama wa Yanga na bahati mbaya Jumanne watamenyana na mahasimu, Simba SC katika Nusu Fainali.
  George Lwandamina (kulia) amekataa kabisa kuuzungumzia mchezo wa jana dhidi ya Azam FC

  Alipoulizwa juu ya mchezo jana, Lwandamina alisema; “Sina cha kusema”. Na alipoulizwa kuhusu mchezo ujao, Lwandamina akajibu pia; “Sina cha kusema”.
  Matokeo hayo yanazifanya timu zote zimalize na pointi saba baada ya kushinda mechi mbili na sare moja, lakini Azam wanakuwa juu ya Yanga kwa wastani wa mabao.
  Sasa Azam itacheza na mshindi wa pili wa Kundi B katika Nusu Fainali, wakati Yanga itacheza na mshindi wa kwanza wa kundi hilo, Simba Jumanne.
  Mabao ya Azam juzi yalifungwa na John Bocco dakika ya pili, Yahya Mohammed dakika ya 54, Joseph Mahundi dakika ya 80 na Enock Atta Agyei dakika ya 85.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: LWANDAMINA 'ABANDIKA PLASTA' MDOMONI Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top