• HABARI MPYA

  Monday, January 16, 2017

  KIPA NAMBA MOJA MTIBWA ASEMA SIMBA HAWACHOMOKI JUMATANO JAMHURI

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  KIPA Said Mohammed Ndunda wa mabingwa wa zamani wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Mtibwa Sugar amesema kwamba watawapunguza kasi Simba SC keshokutwa Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.
  Mtibwa Sugar watakuwa wenyeji wa Simba SC Jumatano Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro katika mfululizo wa Ligi Kuu kuanzia Saa 10: 00 jioni na Ndunda amesema kwamba watashinda mchezo huo.
  Na akizungumza na Bin Zubeiey Sports - Online leo mjini Morogoro, Nduda alisema kwamba Simba SC wataumia Jumatano Uwanja wa Jamhuri. 
  Kipa Said Mohammed amesema kwamba wataipunguza kasi Simba SC Jumatano

  “Naamini tutashinda mchezo huo, kikubwa tu ninawaomba mashabiki wa Mtibwa Sugar wa Morogoro na nje ya Morogoro kwa ujumla waje kwa wingi Uwanja wa Jamhuri siku ya Jumatano kutushabiki mwanzo mwisho. Na wakija kwa wingi kwao ni faraja kubwa kwetu,” alisema Nduda.
  Kipa huyo wa zamani wa Maji Maji ya Songea mkoani Ruvuma na Yanga SC ya dar es salaam amesema kwamba wamejiandaa kikamilifu kushinda dhidi ya Simba kesho.
  “Hatutowaangusha kabisa mashabiki wetu, kama wanavyojua mzunguko wa pili tumeanza vyema hatujapoteza mechi hata moja na tuna uhakika tutafanya vyema kwa kuwa tuna morali na tumejiandaa vyema kuelekea mchezo huo, sisi tunapigana kwa pamoja hivyo lazima tupate matokeo mazuri” alisema Nduda.
  Mechi nyingine ya Ligi Kuu keshokutwa ni kati ya wenyeji Azam FC  na Mbeya City kuanzia Saa 1:00 usiku Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
  Ligi Kuu itaendelea kesho kwa mchezo mmoja tu, kati ya wenyeji Maji Maji ya Songea na Yanga SC Uwanja wa Maji Maji mjini Songea mkoani Ruvuma.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KIPA NAMBA MOJA MTIBWA ASEMA SIMBA HAWACHOMOKI JUMATANO JAMHURI Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top