• HABARI MPYA

  Tuesday, January 17, 2017

  JUMA MAHADHI APANGWA NA TAMBWE MBELE DHIDI YA MAJI MAJI LEO

  Na Mwandishi Wetu, SONGEA
  KOCHA Mzambia wa Yanga, George Lwandamina amemuanzisha kiungo Juma Mahadhi kama mshambuliaji pacha wa Mrundi Amissi Tambwe katika mchezo dhidi ya Maji Maji leo.
  Yanga watakuwa wageni wa Maji Maji Uwanja wa Maji Maji mjini Songea mkoani Ruvuma katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara jioni ya leo.
  Na Lwandamina amepanga kikosi chenye mshambuliaji mmoja tu, Tambwe na viungo watano, ambao ni Thaban Kamusoko, Saimon Msuva, Haruna Niyonzima, Juma Mahadhi na Deus Kaseke.
  Kikosi kamili cha Yanga dhidi ya Maji Maji leo ni; Deogratius Munish 'Dida', Juma Abdul, Haji Mwinyi, Andrew Vincent, Kelvin Yondani, Thaban Kamusoko, Simon Msuva, Haruna Niyonzima, Amissi Tambwe, Juma Mahadhi na Deus Kaseke.
  Katika benchi wapo; Beno Kakolanya, Oscar Joshua, Nadir Haroub 'Cannavaro', Said Juma 'Makapu', Matheo Antony, Yussuf Mhilu na Geoffrey Mwashuiya.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: JUMA MAHADHI APANGWA NA TAMBWE MBELE DHIDI YA MAJI MAJI LEO Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top