• HABARI MPYA

  Friday, January 06, 2017

  JOHN MIKEL OBI NAYE AHAMIA CHINA, ATUA TIANJIN TEDA

  MCHEZAJI wa kimataifa wa Nigeria, John Mikel Obi anakuwa nyota mpya wa Ligi Kuu ya England kuhamia Ligi Kuu ya China akijiunga na klabu ya Tianjin TEDA kutoka Chelsea.
  Mikel, ambaye amejikuta haana nafasi kikosi cha kwanza cha Chelsea msimu huu baada ya kusajiliwa kwa N'Golo Kante, Nemanja Matic, Nathaniel Chalobah na Cesc Fabregas atakuwa analipwa Pauni 140,000 kwa wiki China.
  Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 alikwenda kufanyiwa vipimo jana tayari kumfuata mchezaji mwenzake wa Chelsea, Oscar ambaye amejiunga na Shanghai SIPG.
  Nyota huyo wa Nigeria alikuwa kwenye mazungumzo na klabu za Valencia, Marseille na Inter Milan lakini akaamua kwenda China.
  Mikel amedumu kwa misimu 11 Stamford Bridge baada ya kujiunga kwa utata na Chelsea, licha ya awali kwenda kwenye mkutano na waandishi wa habari Manchester United na kupiga picha na jezi ya klabu hiyo ikiwa na jina lake.
  Inafahamika amesaini mkataba wa miaka mitatu China baada ya kucheza kwa mafanikio makubwa England, akishinda taji la Ligi ya Mabingwa, mawili ya Ligi Kuu ya England na manne ya FA.
  Aliichezea Chelsea mechi za kujiandaa na msimu, lakini baadaye akaenda kujiunga na kikosi chaq Olimpiki cha Nigeria kilichoshinda Medali ya Shaba mjini Rio na tangu hapo hakurejea kwenye mipango ya kocha Antonio Conte.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: JOHN MIKEL OBI NAYE AHAMIA CHINA, ATUA TIANJIN TEDA Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top