• HABARI MPYA

  Thursday, January 12, 2017

  JKT NA RUVU SHOOTING KUUWASHA MOTO LIGI KUU KESHO

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  TIMU za Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Ruvu Stars na Ruvu Shooting zinatarajiwa kumenyana kesho Uwanja wa Mabatini, Mlandizi mkoani Pwani katika mfululizo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
  Mbali ya ‘derby’ ya JKT Ruvu na Ruvu Shooting, Jumamosi Januari 14, 2017 kutakuwa na mchezo mwingine wa upinzani kati ya Stand United na Mwadui FC – zote za Shinyanga na zitapambana kwenye Uwanja wa CCM Kambarage.
  Kadhalika siku hiyo ya Jumamosi Januari 14, 2017 Kagera Sugar itakuwa mwenyeji wa Ndanda FC ya Mtwara kwenye Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba katika mchezo mwingine wa VPL.
  Jumapili Januari 15, 2017 kutakuwa na mchezo mmoja tu wa Ligi Kuu ya Vodacom ambako Mbao itakuwa mwenyeji wa African Lyon ya Mwanza katika mchezo utakaofanyika Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
  Kadhalika Jumatatu Januari 16, 2017 kutakuwa na mchezo mmoja tu ambako Tanzania Prisons itakuwa mgeni wa Toto Africans kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: JKT NA RUVU SHOOTING KUUWASHA MOTO LIGI KUU KESHO Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top