• HABARI MPYA

    Sunday, January 22, 2017

    GYAN AIPELEKA GHANA ROBO FAINALI AFCON, UGANDA YATOLEWA

    MSHAMBULIAJI Asamoah Gyan ameipeleka Ghana Robo Fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika huku Uganda ikiwa timu ya kwanza kuhakikishiwa safari ya kurejea nyumbani baada ya hatua ya makundi.
    Gyan alifunga bao pekee katika mchezo wa kwanza wa Kundi D dakika ya 21 akimalizia krosi ya Jordan Ayew, Black Stars ikiilaza 1-0 Mali.
    Misri ikaitupa nje Uganda kwa bao pekee la mtokea benchi Abdallah El Said dakika ya 89.
    mabingwa mara wa AFCON, Ghana ambao pia ni washindi wa pili wa mwaka 2015 wanakuwa timu ya pili kujihakikishia Robo Fainali hadi sasa baada ya Senegal.
    Michuano hiyo inaendelea leo kwa wenyeji Gabon kumenyana na Cameroon katika mchezo wa Kundi A mjini Libreville ambao wanatakiwa lazima washinde ili kwenda Robo Fainali.
    Wakifungwa watatolewa na wakitoa sare itabidi wasikilizie matokeo ya mechi nyingine ya mwisho ya kundi hilo kati ya Burkina Faso na Guinea-Bissau.
    Rais wa Gabon, Ali Bongo aliwatembelea wachezaji jana na kipa Didier Ovono akasema: "Rais ametupa hamasa kuelekea mechi hiyo. Hiyo itakuwa fainali yetu ya kwanza."
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: GYAN AIPELEKA GHANA ROBO FAINALI AFCON, UGANDA YATOLEWA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top