• HABARI MPYA

  Wednesday, January 04, 2017

  GRANT AWACHUKUA WATOTO WOTE WA PELE KIKOSI CHA AFCON

  KOCHA wa Ghana, Avram Grant ameita wachezaji wanne wapya na kuwabeba watoto wote wa gwiji wa soka wa nchi hiyo, Abedi Pele katika kikosi chake cha wachezaji 26 wa kushiriki michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika Gabon 2017.
  Wanne hao wapya ni pamoja na viungo wawili Ebenezer Ofori na Joseph Larweh Attamah, na washambuliaji wawili, Bernard Tekpetey and Raphael Dwamena.
  Ofori AIK ya Sweden wakati Attamah, mchezaji wa timu ya vijana chini ya umri wa miaka ya Ghana iliyoshinda Kombe la Duniaa la FIFA la U-20 nchini Uturuki mwaka 2013, anachezea Basaksehir F.K. ya Uturuki, ndugu yake asiyejulikana Tekpetey anachezea Schalke ya Ujerumani huku Dwamena amekuwa akitamba kwa mabao Lustenau ya Daraja la Pili Austria.
  Grant alitaja kikosi chake juzi mjini Accra, Ghana kabla ya timu kwenda kuweka kambi ya siku 11 Falme za Kiarabu.
  Katika Kikosi hicho hakuwaita kipa Fatau Dauda, ambaye hivi karibuni amejiunga na Enyimba ya Nigeria na beki wa kushoto wa Leicester City Jeffery Schlupp.
  Nahodha Asamoah Gyan ataongoza kikosi hicho kitakachoshiriki fainali za sita mfululizo za AFCON. Wachezaji wengine maarufu ni watoto wa Ayew, Andre na Jordan; Emmanuel Agyemang Badu, Christian Atsu na Harrison Afful.
  Mabingwa hao mara nne, wamepangwa Kundi D sambamba Misri, Mali na Uganda na wanatarajiwa kwenda Gabon wakati kabisa wa ufunguzi wa mashindano hayo ya 31 ya Afrika.
  Kikosi kamili cha Ghana kinaundwa na makipa; Razak Braimah (Cordoba, Hispania), Adam Kwarasey (Rosenborg, Norway) na Richard Ofori (Wa All Stars).
  Mabeki: Harrison Afful (Columbus Crew, Marekani), Andy Yiadom (Barnsley, England), Baba Rahman (Schalke, Ujerumani), Frank Acheampong (Anderlecht, Ubelgiji), John Boye (Sivasspor, Uturuki), Jonathan Mensah (Anzhi, Urusi), Daniel Amartey (Leicester City, England), Edwin Gyimah (Orlando Pirates, Afrika Kusini). 
  Viungo: Emmanuel Agyemang-Badu (Udinese, Italia), Afriyie Acquah (Torino, Italia), Thomas Partey (Atletico Madrid, Hispania), Mubarak Wakaso (Panathinaikos, Ugiriki), Christian Atsu (Newcastle, England), Ebenezer Ofori (AIK Stockholm, Sweden), Samuel Tetteh (Leifering, Austria), Joseph Larweh Attamah (Başakşehir F.K, Turkey)
  Washambuliaji: Asamoah Gyan (Al Ahli, UAE), Jordan Ayew (Aston Villa, England), Abdul-Majeed Waris (Lorient, France), Andre Ayew (West Ham, England), Ebenezer Assifuah (Sion, Uswisi), Bernard Tekpetey (Schalke, Ujerumani) na Rahpael Dwamena (Austria Lustenau, Austria)
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: GRANT AWACHUKUA WATOTO WOTE WA PELE KIKOSI CHA AFCON Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top