• HABARI MPYA

  Saturday, January 14, 2017

  DRC WAGOMA KUFANYA MAZOEZI, AFCON YAANZA LEO GABON

  WACHEZAJI wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) wamegoma kufanya mazoezi kuelekea mchezo wao wa ufunguzi wa Kombe la Mataifa ya Afrika dhidi ya Morocco kwa sababu ya posho.
  Kiungo wa Norwich City, Yousuf Mulumbu, Nahodha wa DRC (pichani juu) amesema wachezaji waligomea mazoezi jana kwa sababu ya mzozo wa posho.
  "Imekuwa hivi hivi kwa miaka na miaka. Tunajiandaa vizuri kwa mechi zetu na mwishowe wakati wote kuna matatizo ya posho," alisema.
  "Nikisema hivyo, Januari 16 tutapeperusha bendera yetu, katika mchezo wa ufunguzi dhidi ya Morocco,".
  Timu nyingine iliyoingia kwenye mzozo wa posho ni Zimbabwe, ambao walitaka hadi kugoma kuja Gabon ambako wanacheza mechi ya ufunguzi leo.
  Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika zinatarajiwa kuanza leo kwa mchezo kati ya wenyeji Gabon na Guinea-Bissau Uwanja wa Stade d'Angondje Saa 12:00 jioni kabla ya Burkina Faso kumenyana na Cameroon Saa 3:00 usiku.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: DRC WAGOMA KUFANYA MAZOEZI, AFCON YAANZA LEO GABON Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top