• HABARI MPYA

  Thursday, January 19, 2017

  CAMEROON WABISHA HODI ROBO FAINALI, AUBAMEYANG...

  CAMEROON imebisha hodi Robo Fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika baada ya jana kuifunga Guinea-Bissau 2-1, huku wenyeji Gabon wakilazimishwa sare ya pili mfululizo katika Kundi A licha ya Pierre-Emerick Aubameyang kufunga tena.
  Simba Wasiofungika walitoka nyuma na kuifunga Guinea-Bissau kwa mabao ya Sebastien Siani dakika ya 61 na Michael Ngadeu dakika ya 78 baada ya Piqueti Djassi kutangulia kufunga dakika ya 13.
  Cameroon sasa watahitaji sare tu katika mchezo wao wa mwisho na wenyeji Gabon ili kwenda Robo Fainali kutoka Kundi A.
  Katika mchezo uliotangulia, mkwaju wa penalti wa Aubameyang dakika ya 38 uliwanusuru Gabon kulala mbele ya Burkina Faso kwa kupata sare ya 1-1 baada ya Prejuce Nakoulma kutangulia kuwafungia wageni dakika ya 23 Uwanja wa  l'Amitie. 
  Hiyo ilikuwa sare ya pili mfululizo kwa Gabon baada ya kulazimishwa sare ya 1-1 pia dhidi ya Guinea-Bissau.
  Michuano hiyo inaendelea kwa mechi za Kundi B leo, Algeria ikimenyana na Tunisia kuanzia Saa 1:00 usiku na Senegal ikimenyana na Zimbabwe kuanzia Saa 3:00 usiku.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: CAMEROON WABISHA HODI ROBO FAINALI, AUBAMEYANG... Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top